Tanzania na Mauritius kuimarisha ushirikiano katika sekta ya kazi na ajira

0


Balozi wa Tanzania nchini Mauritius, mwenye makazi yake mjini Harare, Zimbabwe, Mhe. CP. Suzan S. Kaganda, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ajira wa Jamhuri ya Mauritius, Mhe. Reza Uteem, katika ofisi za Wizara hiyo nchini Mauritius.

Viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya kazi na ajira, hususan kufungua fursa kwa Watanzania kupata ajira nchini Mauritius katika fani za uuguzi, TEHAMA, huduma za fedha, ufundi na maeneo mengine ambayo wataalamu wake wanapatikana kwa wingi nchini Tanzania.

Aidha, Mhe. Reza Uteem ameeleza utayari wa nchi hiyo kuijumuisha Tanzania katika mpango wa ajira wa nchi hiyo na kuipa kipaumbele katika upatikanaji wa fursa hizo, kwa kuzingatia uhusiano wa kihistoria uliopo baina ya mataifa hayo mawili.

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top