Je unafahamu Sio kila Taarifa Unayoiona Mtandaoni ni ya Kweli? Fahamu Hatua za Kuhakiki Kabla ya Kuisambaza

0

 


Kelvin: “Bro, jana nilijikuta kwenye wakati mgumu sana kwa sababu ya ujumbe mmoja tu wa WhatsApp.”

Mimi: “Ujumbe gani?”

Kelvin: “Nilipokea taarifa kwenye group. Ilisema kuna mabadiliko makubwa yaliyotangazwa na mamlaka fulani. Ujumbe ulikuwa umeandikwa kwa kujiamini kabisa. Watu wengi walikuwa tayari wameusambaza.”

Mimi: “Halafu?”

Kelvin: “Bila hata kujiuliza sana, nikaupeleka kwenye group lingine.”

“Na kumbe?”

“Baadaye nikagundua kuwa taarifa ile haikuwa ya kweli.

Mimi; “Dah! Ulifanya nini?”

“Nilijuta kwa sababu nilikuwa tayari nimeisaidia kusambaa. Sijui watu wangapi wamesoma ujume huo bro”

Hapo ndipo jambo muhimu lilipo.

Changamoto aliyoipitia Kelvin pia inawapata watumiaji wengine wa mitandao ya kijamii wanapopokea taarifa.

Kila siku tunapokea taarifa kupitia WhatsApp, Facebook, TikTok na mitandao mingine. Baadhi ni za kweli. Baadhi ni za uongo. Nyingine zinaweza kuwa na taarifa ya kweli lakini zimepotoshwa.

Kwa hiyo kabla hujabofya Share, fuata hatua hizi:

 1. SUBIRI

Usisambaze taarifa mara tu unapopokea. Chukua muda kwanza. Usitake kuoenekana wewe umekua wa kwanza kupata taarifa na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

2. CHUNGUZA

Jiulize:

  • Nani ametoa taarifa hii?
  • Imetolewa lini?
  • Chanzo cha awali ni kipi?
  • Kuna ushahidi gani?
  • Taarifa hii imeandikwa au kuwasilishwa katika muktadha gani?

3. TAFUTA UTHIBITISHO

Usiegemee ujumbe mmoja tu. Tafuta taarifa hiyo kwenye vyanzo vingine vinavyoaminika. Linganisha taarifa kabla ya kuamua kuisambaza.

Kumbuka:

Ujumbe unaweza kuwa umetumwa na rafiki yako unayemwamini. Lakini hiyo haimaanishi taarifa yenyewe ni ya kweli.

Kabla ya Share, jiulize maswali yafuatayo; Nani amesema? Lini amesema? Chanzo ni kipi? Uthibitisho uko wapi?

Usisambaze taarifa tu. Hakikisha ni taarifa sahihi.

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top