TAKUKURU Yaokoa Shilingi 2.7 Bilioni za Michango ya Wafanyakazi Kagera

0

               

Na Angela Sebastian | Bukoba

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera, imefanikiwa kuokoa zaidi ya Sh2.7 bilioni kati ya Sh5.2 bilioni zilizokuwa zinadaiwa kutoka kwa makampuni binafsi 146 kwa ajili ya michango ya wafanyakazi wao katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera, Ismail Bukuku, amesema hayo Septemba 16, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Bukoba, akieleza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya taasisi hiyo kufanya ufuatiliaji dhidi ya waajiri waliokuwa hawawasilishi michango ya wafanyakazi kwa wakati.

Kwa mujibu wa Bukuku, waajiri hao walikuwa hawajalipa michango hiyo kwa kipindi cha miaka tisa, kuanzia mwaka 2017 hadi Julai 2026, ambapo jumla ya Sh 5.2 bil. zilikuwa zinadaiwa.

Amesema katika awamu ya kwanza ya ufuatiliaji, TAKUKURU iliweza kuokoa Sh1.6  bil sawa na asilimia 31 ya fedha zilizokuwa zinadaiwa.

Aidha, katika awamu ya pili ya operesheni hiyo, timu ya ufuatiliaji ilifanikiwa kuokoa zaidi ya Sh1 bilioni, na kufanya jumla ya fedha zilizookolewa kufikia zaidi ya Sh2.7 bil sawa na asilimia 52 ya deni lote.

Bukuku amesema operesheni hiyo ilifanyika kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza ilianza Julai 22 hadi Agosti 5, 2026, huku awamu ya pili ikifanyika kuanzia Agosti 17 hadi Agosti 31, 2026.





Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top