Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mara moja ya majukumu yake ni ufuatiliaji wa fedha za umma zinazotolewa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo..
Katika kutekeleza jukumu hilo ilifanikiwa kupata taarifa ya mkandarasi aliyekua akifanya kazi ya ukarabati wa barabara ya majita iliyopo manispaa ya Musoma mkoani Mara, kutekeleza kazi ya kuziba mashimo kwenye barabara ya lami chini ya kiwango ilianza ufuatiliaji na kubaini uwepo wa dosari na hivyo kuchukua hatua ya kuzuia malipo ya fedha shilingi milioni thelathini na nane za mkandarasi na kumtaka mkandarasi kurudia kazi hiyo.
Mayunga Selestine ni afisa wa TAKUKURU katika dawati la Kuzuia na Kupambana na rushwa mkoa wa Mara ameyasema hayo wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari mkoa wa Mara ambapo amesema moja ya majukumu ya taasisi hiyo ni ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma zinazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na endapo wakipata taarifa uanza uchunguzi mara moja na endapo wakibaini changangamoto katika utekelezaji wa miradi hiyo uchukua hatua kwa wahusika ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani..
Kwa upande wake Naibu wa Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mara Sadiki Nombo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za matumizi mabaya ya fedha za umma katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali, ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa wa sheria ambapo mbali na hukumu pia sheria inaelekeza watuhumiwa wanaobainika kutenda kosa utakiwa kurejesha fedha za miradi.







