Tiba Utalii Kuchochea Ukuaji wa Uchumi Nchini

0


Na Mvuda Jaffer, WAF - Dodoma

Serikali imepiga hatua katika kuimarisha sekta ya utalii wa matibabu (Medical Tourism) inayotarajiwa kuongeza mchango wa sekta ya afya katika ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja na kuvutia wagonjwa kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Ameeleza hayo Mratibu wa Tiba Utalii wa Wizara ya Afya, Dkt. Asha Mahita leo Mei 21, 2026 katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wauguzi Viongozi unaofanyika mkoani Dodoma 

“Imeelezwa kuwa duniani kote, ifikapo mwaka 2032 sekta ya "medical tourism" inatarajiwa kuzalisha zaidi ya dola za Marekani bilioni 100, hali inayozifanya nchi mbalimbali kuendelea kuwekeza katika huduma bora za afya, miundombinu ya kisasa pamoja na mifumo ya kuvutia wagonjwa kutoka nje ya nchi.” amesema Dkt. Mahita

Dkt. Mahita ameongeza kuwa, kwa sasa Tanzania imeanza kupokea wagonjwa kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika ikiwemo Comoro, Uganda, Angola, Malawi na Zambia ambapo wamekuwa wakifika kupata huduma katika hospitali za umma na binafsi.

Aidha, Dkt. Mahita amefafanua kuwa medical tourism siyo tu suala la mgonjwa kusafiri kwa ajili ya matibabu, bali pia linajumuisha huduma nyingine muhimu kama mapumziko, ushauri wa afya, huduma za ustawi wa mwili na akili pamoja na tiba mbadala zinazosaidia kuboresha afya kwa ujumla.

“Kuna tofauti kati ya wagonjwa wanaokuja moja kwa moja kutafuta huduma nchini na wale wanaopelekwa kupitia mfumo wa rufaa kutoka Hospitali au nchi nyingine, huku mfumo huo wa rufaa ukitajwa kuwa sehemu muhimu ya kukuza sekta ya tiba utalii nchini.”ameongeza Dkt. Mahita

Sambamba na hilo, Dkt. Mahita ameeleza Tanzania imeanza kushuhudia ongezeko la huduma za “reverse medical tourism” ambapo wataalamu wa afya kutoka nje ya nchi wanakuja nchini kutoa huduma maalumu za kibingwa kwa kutumia miundombinu ya ndani.

“Bado kuna nafasi kubwa ya kuwekeza katika huduma za wellness ikiwemo vituo vya meditation, yoga, recreation pamoja na tiba mbadala ambazo zinaweza kuongeza mvuto wa Tanzania katika soko la kimataifa la medical tourism,” wameeleza wataalamu wa afya.


Katika kuimarisha sekta hiyo, viongozi wa afya wametakiwa kusaidia ukusanyaji wa takwimu sahihi za wagonjwa wa kimataifa wanaopata huduma katika vituo vya afya nchini ili kuwezesha upangaji wa mikakati bora ya maendeleo ya sekta hiyo pamoja na kuongeza mchango wake katika uchumi wa taifa.


Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top