AFDP Yawajengea Uwezo Wauzaji wa Pembejeo 200

0


Wizara ya Kilimo kupitia Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayotekelezwa hapa nchini kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD) imetoa mafunzo kwa wauzaji wa pembejeo zaidi ya 200 katika Mikoa ya Morogoro na Manyara kwa lengo la kuwajengea uwezo ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

Mafunzo yameendeshwa tarehe 11-15 Mei 2026 na wataalamu kutoka Taasisi ya Uthibiti wa Ubora wa Mbegu (TOSCI), Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania(TFRA), Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Wakala wa Mbegu za Kilimo(ASA) na Maafisa kutoka Wizara ya Kilimo.

Watafiti na Wathibiti wa ubora wa mbegu kutoka TOSCI wametoa mafunzo kwa wauzaji wa pembejeo kuhusiana na utunzaji wa mbegu, mbinu bora za uuzaji wa mbegu pamoja na namna ambavyo wafanyabiashara hao wanavyoweza kushirikiana na TOSCI katika kufichua wauzaji wanaokiuka sheria na taratibu za biashara ya mbegu.  Pia wamefundishwa mbinu za kutambua mbegu zisizokuwa na ubora stahiki ambazo zimekuwa ni kero kwa wakulima na kuwasisitiza kuwa wanatakiwa kuuza mbegu zilizothibitishwa na Taasisi ya Uthibiti wa Ubora wa Mbegu (TOSCI).

Kwa upande wa TFRA, mafunzo yalijikita katika kutoa elimu ya matimizi sahihi ya mbolea.  Vile vile, TPHPA ilitoa msisitizo wa kuepuka wadanganyifu wanaenda madukani kwa kujitambulisha kuwa ni maafisa wakaguzi lakini wengi wao ni matapeli. 

Akizungumza kwa niaba ya Mratibu wa Programu ya AFDP, Afisa kutoka , Bw. Ernest Kibulei amewataka wafanyabiashara hao kuhakikisha wanatoa huduma bora, zenye ubora na zinazokidhi mahitaji ya wakulima, ambao ni wadau muhimu katika maendeleo ya sekta ya kilimo na shughuli zao za biashara.

✍️wizara ya kilimo

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top