#MatukioKatikaPicha
Uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Maadili na Malezi Chanya kwa Watoto yenye kaulimbiu isemayo “Mtoto ni Malezi; Msingi wa Familia Bora kwa Taifa Imara.” (Tuanzie nyumbani) ambapo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mheshimiwa Dkt. Dorothy Gwajima, amezindua
Kampeni hiyo inayolenga kuhamasisha wazazi, walezi na jamii kuhusu umuhimu wa malezi chanya, maadili mema na ulinzi wa watoto dhidi ya ukatili pamoja na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, ambapo itatekelezwa nchi nzima hadi Juni 30, 2026.
Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 24, 2026 wilayani Handeni mkoani Tanga kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
chanzo: maendeleo ya jamii









