Serikali kusajili data za Tiba Asili kwenye mfumo rasmi wa ugavi wa MSD

0


Na Aisha Swahibu, WAF - Dodoma

Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amemtaka Mfamasia Mkuu wa Serikali kusaidia kuandaa utaratibu wa kitaalamu utakaowezesha dawa za tiba asili zinazokidhi viwango vya ubora, usalama na masharti ya udhibiti ubora kuingizwa katika mnyororo wa ugavi wa dawa na vifaa tiba kupitia Bohari ya Dawa (MSD).

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo, Machi 25, 2026, wakati wa kikao chake na wataalamu wa tiba asili kilichofanyika jijini Dodoma, chenye kauli mbiu isemayo: “Kuimarisha huduma za tiba asili zenye ushahidi wa kisayansi.”

Amesema hatua hiyo ni muhimu ili kuhamisha tiba asili kutoka pembezoni mwa mfumo wa afya kwenda kwenye mfumo rasmi wa upatikanaji wa huduma.

Aidha, ameitaka Idara ya Tiba kushirikiana kwa karibu na Taasisi ya inayosimamia na kuratibu masuala yote ya sayansi, teknolojia na utafiti nchini (COSTECH) kutambua, kulea na kukuza wagunduzi na wabunifu wa tasnia ya tiba asili.

“Hatua hii itawezesha mawazo yao kufikishwa kwenye tafiti, uthibitishaji, ubunifu wa bidhaa, biashara na hatimaye viwanda,” amesema Mhe. Mchengerwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mchengerwa amesema Wizara ya Afya kwa kushirikiana na taasisi husika inapaswa kuanza mara moja maandalizi ya kuanzisha mfumo wa kitaifa wa kidijitali wa taarifa za tiba asili. Mfumo huo utasaidia katika utunzaji wa maarifa, ufuatiliaji wa usalama, ukusanyaji wa ushahidi pamoja na kuharakisha tafiti, ubunifu na usimamizi wa sekta hiyo kwa ufanisi zaidi

✍️wizara ya afya







Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top