Tanzania Mwenyeji wa warsha ya Kanda ndogo ya shirika la mawasiliano duniani (ITU) kwa Africa

0


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari akizungumza kwenye ufunguzi wa Warsha ya Kanda ndogo ya Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) kwa Afrika (ITU Subregional Workshop for Africa), inayofanyika katika hoteli ya Ramada jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 24 hadi 26 Machi, 2026.

Warsha hiyo inawakutanisha wataalamu kutoka nchi 23 za Afrika zinazozungumza lugha ya Kingereza, kujadili kuhusu kukuza upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa nchi wanachama na kuimarisha matumizi yenye tija kwa wote (Promoting and Measuring Universal and Meaningful Connectivity (UMC).

Akizungumza kwenye ufunguzi wa warsha hiyo, Dkt. Bakari amesema, Tanzania inaendeleza jitihada za kuongeza ufikiwaji jumuishi wa huduma za mawasiliano yenye tija kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), na kuboresha  mazingira ya kiudhibiti yanayounga mkono na kuenda sambamba na jitihada za kukuza na kupima upatikanaji wa mawasiliano yenye tija kwa watumiaji wote ili kuongeza athari chanya za kijamii na kiuchumi.

Warsha hii ya siku tatu inahusisha washiriki kutoka kada mbalimbali kama vile taasisi za ukusanyaji wa takwimu, taasisi zinazofanya tafiti, mamlaka za udhibiti wa mawasiliano kwa nchi za Afrika, taasisi za elimu ya juu, watoa huduma za mawasiliano pamoja na Wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Tanzania.

Tanzania kupitia Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ni mwenyeji wa warsha hii, ikiratibu kwa kushirikiana na Ofisi ya Maendeleo ya Mawasiliano ya Shirika la Mawasiliano Duniani (BDT).

✍️tcra

#tcratz #itu #itusburegional #meaningfulconnectivity

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top