NEMC Yatoa mafunzo ya utunzaji wa maeneo ya milima

0


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais jana Machi 24, 2026 wameendesha mafunzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino juu ya uhifadhi na usimamizi wa maeneo ya milima.

Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri na kufunguliwa na Dkt. Caren Kahangwa ambaye ni Meneja wa Maeneo Maalum na Mabadiliko ya Tabianchi kwa niaba ya Mkurugenzi wa NEMC.

Mafunzo hayo yaliwashirikisha maafisa mazingira, maafisa mipango miji pamoja na watendaji na wenyeviti wa vijiji vya Dabalo, Nayu, Itiso, Solowu, Membe, Nzali na Kawawa vinavyopatika katika Wilaya ya Chamwino na kijiji cha Mkondai kutoka Wilaya ya Bahi. Aidha kwa upande wa Jiji la Dodoma yalishirikisha mitaa ya Msisi, Maseya na Mkoyo.

Wadau wengine walioshiriki katika mafunzo hayo ni pamoja na Tume ya Madini, Bonde la Maji la Wami Ruvu, Taasisi ya Jiolojia, Utafiti wa Madini, Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma na Wakala wa Huduma za Misitu.

Aidha, mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wadau, maafisa na wenyeviti hao juu ya namna bora ya kutunza na kutatua changamoto zinazotokana na utunzaji wa maeneo ya milima.

Sambamba na hilo, washiriki wa mafunzo hayo watapata nafasi ya kufanya tathmini ya usimamizi wa mfumo ikolojia ya mlima Chinyami unaopatikana katika Wilaya ya Chamwino.

✍️nemc








Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top