Rhobi Samwelly awataka wanawake kutumia fursa zinazowazunguka kujikwamua kiuchumi

0


Na Mwandishi Wetu, Rorya. 

Mkurugenzi wa shirika lisilo la  Kiserikali la Hope for Girls and Women in Tanzania linalojishughulisha na kupambana na ukatili wa Kijinsia Mkoani Mara Rhobi Samwelly, amewataka Wanawake  kuendelea kuzitumia vyema fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwa ni pamoja na  mafunzo ya ujasiriamali na mikopo nafuu  inayotolewa na Serikali kusudi waweze kujiletea maendeleo. 

Ameyasema hayo   Machi 6, 2026,  alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Wilayani  Rorya Mkoani Mara. 

Maadhimisho hayo yamefanyika kata ya Koryo katika  uwanja wa Shule ya Msingi utegi na kuhudhuriwa na makundi mbalimbali ya Wanawake kutoka Sekta binafsi, taasisi za umma, serikalini  pamoja na Wananchi Wilayani humo.

Ambapo  kauli mbiu ya mwaka huu inasema 'Haki kwa Wanawake na Wasichana, Msingi wa maendeleo jumuishi kufikia Dira 2050'

Rhobi amesema, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Hassan  imeendelea Kutoa fursa ya mikopo nafuu kwa wanawake, hivyo ni muhimu wakachangamkia fursa hiyo ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kufanya  shughuli za biashara na ujasiriamali. 

Pia,  amewataka wanawake Wilayani humo, kutumia siku hiyo kujitathmini na kuimarisha malezi bora kwa watoto wao kwani wana nafasi nzuri kuimarisha  malezi, makuzi sambamba na  kusimamia maadili mema yatakayowasaidia watoto kukua katika mazingira salama na yenye heshima.

Pia, amesisitiza wanawake  kujiepusha na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, akieleza kuwa ukatili unaathiri maendeleo ya watoto kimwili, kiakili na kisaikolojia. Huku akihimiza  wazazi na walezi kuwalinda watoto na kuwapa malezi yenye upendo  wakizingatia haki za watoto ili kuwasaidia kufikia ndoto zao za baadaye.

"Wanawake tukijiimarisha kiuchumi tutaweza kusaidia familia zetu, kuwapatia watoto mahitaji muhimu na kuchangia maendeleo ya jamii na Taifa letu kwa  ujumla."amesema Rhobi. 

Akisoma risala ya Wanawake wa Wilaya ya Rorya  Lilian Fransisco ambaye ni Mratibu wa Dawati la Wanawake Wilaya ya Rorya amesema anaipongeza serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuwathamini Wanawake na kutatua changamoto zao mbalimbali.




Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top