Balozi Luvanda aipongeza NEMC kwa uwajibikaji wenye tija

0


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Balozi Baraka Luvanda, amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa uwajibikaji wenye tija katika kutekeleza majukumu yake ya kuhifadhi na kusimamia mazingira nchini.

Ametoa pongezi hizo leo alipozuru Ofisi za Baraza zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ikiwa ni ziara yake ya kwanza kwa watumishi wa NEMC tangu kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo. 

Alisema lengo la ziara yake ni kukutana na kuzungumza na watumishi wa Baraza hilo pamoja na kuonesha azma yake chanya ya kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya sekta ya mazingira nchini, hasa ikizingatiwa kuwa mazingira ni eneo muhimu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambapo ni mhimili wa tatu katika maendeleo ya taifa.

“Nimefurahi sana kuona mkitekeleza majukumu yenu kwa ufanisi. Sina shaka maana najua sitakwama mahali popote , mahali hapa pamesheheni wawajibikaji wenye uzalendo wa mazingira nchini mwetu, Tambueni mmepewa jukumu kubwa kwa nchi hii; Mheshimiwa Rais anawaangalia nyinyi zaidi,” alisema.

Aliongeza kuwa watumishi wa NEMC wanapaswa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uadilifu katika kusimamia rasilimali za mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

“Nyinyi sio wadogo. Mmeonesha kuwa mnaweza kutimiza wajibu wenu kwa uadilifu. Nimefurahi kuona maadili ya kazi yakizingatiwa,” alisisitiza.

Awali, akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu na kutambulisha safu ya watumishi wa NEMC, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt Immaculate Sware Semesi alieleza kuwa NEMC kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 na Kanuni zake, imekasimiwa  majukumu ya utekelezaji ambayo ndio msingi mzima wa mazingi

Alitaja majukumu hayo kuwa ni kusimamia na kulinda mazingira, kufanya Tathmini ya Athari kwa mazingira (EIA), kufuatilia na kukagua miradi ya maendeleo, kutoa elimu na uhamasishaji wa mazingira, kushauri Serikali kuhusu masuala ya mazingira, kudhibiti uchafuzi wa mazingira, kupokea na kushughulikia malalamiko ya mazingira na kuratibu utekelezaji wa sheria za mazingira

Dkt. Sware alimhakikishia Naibu Katibu Mkuu huyo kuwa watumishi wa NEMC wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kemp ushirikiano wote unaohitajika ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu ya Taifa.

✍️nemc









Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top