Rhobi Samwelly ahimiza ushirikiano kuondoa vikwazo vinavyowakabili watoto wa kike

0


Na Mwandishi Wetu, Musoma. 

IMEBAINISHWA kuwa, juhudi za kuondoa vikwazo vinavyowazuia baadhi ya watoto wa kike Mkoani Mara  kufikia ndoto zao haziwezi kuachwa mikononi mwa serikali pekee, bali ni jukumu la kila mwananchi kwa nafasi yake, kwa lengo la kujenga jamii yenye ustawi na taifa lenye maendeleo endelevu.

Akizungumza Machi 19, 2026 na Musoma News Hub, Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Hope for Girls and Women in Tanzania, Rhobi Samwelly, amesema kuwa ipo haja ya mshikamano wa pamoja katika kupambana na changamoto zinazowakumba watoto wa kike hasa maeneo ya vijijini. 

Amebainisha kuwa,  baadhi ya vikwazo vinavyoathiri ustawi wa watoto wa kike ni pamoja na ukeketaji, ndoa za utotoni na vitendo vya manyanyaso ya kijinsia. Hivyo mshikamano madhubuti lazima uwepo miongoni mwa Wananchi kuweza kuviondoa. 

“Sote tushirikiane kuondoa vikwazo vinavyowakabili baadhi ya watoto wa kike katika Mkoa wetu wa Mara. Pia tuwawezeshe kwa kuwapa mahitaji muhimu na kuwatia moyo ili waweze kufikia ndoto zao kimaisha kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla,” amesema Rhobi.

“Tusiiachie serikali au wadau pekee jukumu la kupambana na mila kandamizi. Ni wajibu wetu sote kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu, wanapatiwa mahitaji yao ya msingi, wanafuatiliwa kwa karibu kimasomo,  wanatiwa moyo  na wanapata fursa sawa kama watoto wa kiume.” amesema.

Ameongeza kuwa, Watoto wa kike wanayo fursa nzuri ya kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika Jamii. Hivyo, mila kandamizi dhidi yao zisipewe nafasi ya kudhoofisha safari ya kufikia ndoto zao kimaisha.

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top