Jeshi la Polisi Kagera lapiga marufuku disco toto Eid na Pasaka

0


 Na Angela Sebastian 

Bukoba : Jeshi la polisi mkoani Kagera limepiga marufuku disco la watoto wakati wa kusherekea sikukuu za Eid na Pasaka ili kuwaepusha na madhara ambayo yamekuwa yakijotokeza siku za nyuma pindi wanapokuwa kwenye kumbi za disco hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari, kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera Blasius  Chatanda leo ofisini kwakwe amesema jeshi hilo mpaka sasa hawajapaokea taarifa kutoka kwa mtu yoyote ya kuomba kibali ili kuendesha biashara hiyo ya disco toto hivyo, ni marufuku mtu yeyote kufanya hivyo.

Amesema malezi na ulinzi wa mtoto unaanzia  nyumbani hivyo amewataka wazazi na walezi kutowaachia watoto kwenda matembezi pake yao siku hizo kwa ajili ya kulinda usalama wao,pia amewataadhalisha watu wote kutoendesha magari wakiwa wamelewa na endapo watabainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua kali kwa mijibu wa sheria.


Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top