Mahenge Spinel : fursa ya uwekezaji wa kipekee katika soko la Vito duniani

0


Spinel ni miongoni mwa madini ya vito yenye thamani kubwa sana duniani, yanayoendelea kupata umaarufu mkubwa katika masoko ya kimataifa kutokana na ubora wake wa kipekee, rangi adimu na uimara wa hali ya juu. Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani zilizojaaliwa rasilimali hii adimu, hususan katika eneo la Mahenge, Kijiji cha Epanko, Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro, eneo ambalo limejijengea sifa ya kuwa chanzo cha spinel bora zaidi duniani.

Spinel ni jiwe la vito lenye rangi mbalimbali ikiwemo nyekundu, pinki, zambarau, bluu na machungwa. Umaarufu wake unatokana na sifa kadhaa muhimu ikiwemo uwazi wake wa hali ya juu (high clarity), rangi kali na ya kuvutia inayopendwa sana katika soko la vito, pamoja na uimara mkubwa unaoufanya kudumu kwa muda mrefu. Aidha, spinel nyingi hupatikana bila kuhitaji matibabu ya joto (heat treatment), jambo linaloongeza thamani yake sokoni.

Kwa miaka mingi, spinel nyekundu ilichanganywa na ruby hadi pale sayansi ya madini ilipobaini tofauti zake. Leo hii, spinel imesimama kama jiwe la vito lenye hadhi yake binafsi na thamani inayozidi kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Mahenge, iliyopo Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, ni eneo lenye umuhimu mkubwa katika ramani ya madini ya vito duniani. Spinel inayopatikana Mahenge inajulikana kwa rangi yake ya pinki na nyekundu yenye mwanga wa kipekee (neon-like glow), sifa inayofanya spinel ya Mahenge kutafutwa sana na wafanyabiashara wa vito duniani.

Ugunduzi wa spinel katika eneo hili umeifanya Mahenge kutambulika kimataifa na kuiweka Tanzania miongoni mwa nchi muhimu katika biashara ya madini ya vito. Spinel ya Mahenge imekuwa ikitajwa mara kwa mara katika maonesho makubwa ya vito ya kimataifa ikiwemo Tucson Gem Show nchini Marekani, Hong Kong Jewellery Fair, pamoja na maonesho ya vito ya Bangkok, Thailand, hatua inayoongeza hadhi ya Tanzania katika soko la kimataifa la madini ya vito.

Uchimbaji wa spinel Mahenge unaongozwa na kampuni za Kitanzania, zikiwemo Ruby International Limited na Franone Mining, ambazo ndizo wawekezaji wakuu katika uchimbaji wa madini haya katika eneo hilo...

✍️wizara ya madini











Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top