Dkt. Gwajima : Nishati safi ya kupikia ni mkombozi wa mwanamke na uchumi wa kaya

0


Na Saidi Saidi – WMJJWM, Dar Es Salaam

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia ni nyenzo muhimu ya kumkomboa mwanamke, kuboresha afya za familia na kuchochea maendeleo ya uchumi wa kaya.

Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Wanawake wa TANESCO linalolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Kongamano hilo lililowakutanisha wanawake wa TANESCO kutoka mikoa yote nchini, limefanyika tarehe 4 Machi 2026 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Dkt. Gwajima amelipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupitia kampeni matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa umeme inayolenga kubadili mtazamo wa jamii na kuongeza matumizi ya umeme katika shughuli za kila siku, hususan kupikia. 

Akizungumza katika kongamano hilo, Waziri Gwajima Amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeweka ajenda ya nishati safi ya kupikia kuwa kipaumbele cha kitaifa, ikilenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ifikapo mwaka 2034.

Katika hatua nyingine, Dkt. Gwajima ameahidi kuwa Wizara itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa TANESCO kupitia kampeni za uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, akisisitiza kuwa ajenda hiyo inagusa moja kwa moja maendeleo ya jamii, hususan wanawake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, amesema lengo la kampeni hiyo ni kubadili mtazamo wa jamii na kuongeza matumizi ya umeme katika shughuli za kila siku, hususan kupikia huku akisisitiza kuwa TANESCO itaendelea kuzingatia usawa wa kijinsia katika utekelezaji wa mipango na miradi yake ili kuendana na malengo ya Dira ya Taifa ya 2050, pamoja na kukuza ushiriki wa wanawake katika sekta ya nishati.

✍️maendeleo ya jamii










Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top