Wataalamu Sekta ya Ardhi Watakiwa Kuvaa Vitambulisho vya Kazi Wakati Wote Wanapotoa Huduma

0


👉 Vitambulisho hivyo ni tiba dhidi ya utapeli kwenye sekta ya Ardhi 

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya amewataka wataalamu wa sekta ya Ardhi nchini kuhakikisha wanavaa vitambulisho vya utambuzi wao wakati wanapokuwa katika vituo vyao vya kazi na uwandani ambapo huduma za masuala yahusuyo ardhi zinatolewa .

Naibu Waziri Mmuya ameyasema hayo leo tarehe 20 Februari 2026 alipotembelea Kliniki ya Ardhi inayoendelea katika eneo la viwanja vya Mji Mwema Kigamboni jijini Dar es Saalam.

Amesema kuwa utaratibu huo utasaidia kuwabaini watu wasioitakia mema sekta ya ardhi nchini kwa kujifanya ni watumishi wa sekta hiyo ambapo imedaiwa wamekuwa wakiwalaghai wananchi kwa kuwapatia huduma hewa wanapofika katika ofisi za ardhi.

"Watumishi wote wa Ardhi ndani ya Sekta ya Ardhi popote mnapotoa huduma, hakikisheni mnavaa vitambulisho vyenye majina yenu tena kutambulisho halali cha serikali bila kificho", amesema Naibu Waziri Kaspar Mmuya.

Kliniki hiyo imeanza February 16 na itamalizika February 28,2026 ikilenga kuwahudumia wakazi wa Kigamboni kwa kutatatua kero zao za ardhi na kupewa Hatimiliki.

✍️wizara ya ardhi

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top