Serikali yasisitiza upangaji ardhi ili kudhibiti migogoro ya Vijiji

0


Serikali imezitaka halmashauri zote nchini kutenga fedha katika bajeti zao kwa ajili ya kuandaa na kutekeleza mipango ya matumizi bora ya ardhi, hatua inayolenga kudhibiti migogoro ya mipaka ya vijiji, kulinda rasilimali za ardhi na kuweka msingi imara wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

Hayo yamesemwa mapema leo tarehe 24 Februari 2026 na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya katika kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Lindi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kikiwa na lengo la kujadili namna ya kuboresha miundombinu ya barabara ambapo sekta ya ardhi ni kiungo muhimu.

Mhe. Mmuya amesema kuwa kutekelezwa kwa mpango huo ambao ni dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameelekeza kila kipande cha ardhi nchini kipimwe na kumilikishwa utaondoa migogoro ya mipaka baina ya wananchi na Vijiji.

"Mmepewa maelekezo nafahamu Katika kila halmashauri mtenge fedha kwa ajili ya Kupanga Kupima na Kumilikisha" amesema Naibu Waziri Kaspar Mmuya. 

"Migogoro mingi ya vijiji inatokana na baadhi ya vijiji kutokuwa na mpango wa matumizi ya ardhi " amesema Naibu waziri Kaspar Mmuya.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi. Zainab Telack amesema kuwa mkoa wake umejipanga kuongeza wigo wa makusanyo ya ndani ili kuweza kufanikisha mpango wa kupima kupanga na kumilikisha ardhi.

"Kila unapokayanga ardhi, ardhi na sisi umetuusia, kwa hiyo ninauhakika utulivu utakwenda kuwepo" amesema Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

✍️wizara ya ardhi

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top