Rhobi Samwelly Awataka Wazazi Waimarishe Malezi, Maadili Kujenga Kizazi Bora

0


Na Mwandishi Wetu, Musoma. 

WAZAZI  na walezi wamehimizwa kuendelea kusimamia kikamilifu malezi na maadili ya watoto wao, wakitambua kuwa jukumu hilo ni muhimu katika kujenga kizazi chenye maadili mema na mustakabali mwema wa Taifa.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT), linalojishughulisha na kupambana na ukatili wa kijinsia mkoani Mara, Rhobi Samwelly,  ameyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na Musoma New Hub

Rhobi amebainisha kuwa uwajibikaji wa wazazi na walezi ni nguzo muhimu katika kujenga kizazi bora na endelevu, sambamba na kuimarisha upendo, ulinzi na makuzi bora kwa wato.

“Wazazi na walezi, tuendelee kutimiza wajibu wetu kikamilifu ili kujenga kizazi bora. Tuwape watoto wetu malezi bora yatakayochangia kujenga Taifa thabiti. Tusiwafanyie vitendo vya ukatili vinavyoathiri maisha yao,  badala yake, tuhakikishe wanapata elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya baadaye,” amesema Rhobi.

“Mila zenye madhara kwa watoto wa kike tuzipige vita kwa umoja wetu, ikiwemo ukeketaji, ndoa za utotoni na ajira za umri mdogo kwa watoto wa jinsi  zote. Tushirikiane na serikali pamoja na wadau wote wa afua za kupinga ukatili ili kuimarisha ustawi bora wa watoto bila upendeleo,” amesema  Rhobi.

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top