Hatutaki Watumishi wa Sekta ya Ardhi Kuwa Sehemu ya Matatizo - Dkt. Akwilapo

0


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo amesema wizara yake haitaki watumishi wa sekta ya ardhi kuwa sehemu ya migogoro ya ardhi nchini.

Mhe. Dkt Akwilapo ametoa kauli hiyo tarehe 22 Desemba 2025 wilayani Masasi wakati alipowasili wilayani Masasi na kupokelewa kwa mara ya kwanza tangu ateuliwa kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

"Kuanzia sasa hatutaki mtumishi wetu awe sehemu ya tatizo tukigundua wewe mtumishi wa sekta ya ardhi umekuwa sehemu ya tatizo basi wewe siyo mfanyakazi wetu na hilo tutalisimamia". Amesema

Amebainisha kuwa, matatizo ya ardhi yapo na yanatengenezwa na watumishi wa sekta ya ardhi pamoja na wananchi ambapo ameweka wazi kuwa, matatizo yaliyotengenezwa basi wizara yake itayatatua.

"Hatupendi kufukuza kazi watumishi maana tunajua kila mfanyakazi anategemewa na kumfukuza itakuwa kitu cha mwisho lakini kuna mahali inabidi sheria ifuate mkondo wake.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo yupo wilayani Masasi mkoa wa Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine atakutana na wananchi wa jimbo lake kwa lengo la kusikiliza na kizitafutia ufumbuzi changamoto mablimbali jimboni humo.

Chanzo: wizara ya ardhi

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top