Kijiji cha Buzi Sasa ni Salama Njooni Tuwekeze Nyumbani - Edwin Mugoha

0


 Na Angela Sebastian 

Bukoba: WAZAWA wa kijiji cha Buzi kata ya Buzi iliyopo Wilayani Bukoba mkoani Kagera wamewaomba wenzao walioko ndani na nje ya nchi  kuondokana na wasiwasi wa imani za kishirikiana ambazo ziligubika kijiji hicho huko nyuma na kuja kuwekeza na kuleta maendeleo.

Edwin Mugoha ni mwenyekiti wa umoja wa Wanabuzi waishio nje na ndani ya Tanzania  (Buzi Development Community-BUDECO)  ambapo amesema kwa kipindi cha miaka minne sasa wamedhamilia kuweka mkakati madhubuti wa kuunda chama ambacho kinaunganisha wanabuzi wa ndani na nje ili kurudi nyumbani na kuondoa fikra potofu kwa kukuza uchumi wa nyumbani kwao.

Mugoha alisema hayo  jana wakati  wa madhimisho ya Buzi day ambayo imeadhimishwa kijijini humo na kuudhuliwa na viongozi mbalimbali na watumishi wa Serikali,wadau kutoka maeneo mbalimbali na wanachama wenyewe.

"Chama chetu chenye wanachama 60 wa kuanzia walioko ndani na nje ya nchi tumerudi nyumbani ili kuijenga Buzi yetu sisi wenyewe kwa kushirikiana na Serikali kwa kuwaondoa hofu watu kuwa sehemu hii ni salama hakuna uchawi wa aina yoyote maana ata wafanyakazi walioletwa na Serikali kufanya kazi hapo waliacha kazi na kukimbia kwa kuhofia usalama wao jambo ambalo ilikuwa uzushi tu ambao ulienea na kuleta sifa mbaya ndani na nje ya mkoa wa Kagera"alisema Mugoha.

Alisema kuwa kutokana kijiji hicho kuwa na sifa mbaya huko nyuma wameamua kurudi kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo itakayovutia uwekezaji ikiwemo vyumba vya madarasa,maabara,barabara,kulipia umeme na kuwaingizia Umeme kwenye nyumba za watu wasiojiweza ikiwa ni sambamba na mpango wa muda mrefu wa kuhakikisha wanagharimia masomo kwa watoto wenye familia zisizojiweza.

"Kijiji hiki kilitengenezewa picha mbaya kama vile Sumbawanga ambapo waliitwa wachawi lakini hivi leo watu wengi wametoka pande mbalimbali za nchi na kwenda kuwekeza huko pia ni matajiri kwahiyo sifa ya uchawi imefutika hivyo, na sisi tumedhamilia umaskini na sifa mbaya kwa Buzi basi kinachofuata ni kuinua uchumi wetu na kuleta maendeleo"alisema

Alisema  sasa hivi walimu,watendaji hata wachungaji wamekubali kwenda kufanya kazi huko ukilinganisha na siku za nyuma.

Alisema kwasasa chama chao wameanzisha mashamba mbalimbali ya uwekezaji katika kijiji hicho ambapo wanatarajia kupanda mikahawa ambalo ni zao la Biashara la mkoa wa Kagera,kupanda mpunga na mbogamboga za majani kwani kijiji hicho kinazungukwa na tingatinga lisilokauka maji hivyo itakuwa rahisi kumwagilia muda wote watakapopanda mazao na kutoa matunda bora zaidi.

Kwa upande wa mwenyekiti wa kijiji cha Buzi Peterson Rwiza amewashukuru Budeco kwa dhana yao ya kuunganisha kijiji hicho katika ramani ya mafanikio kutokana ma miradi waliyoitekeleza kwa kushirikiana na  Serikali hususani ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa ambavyo vimesababisha watoto kuepuka kuvuka msitu na tingatinga lenye wanyama wakali kwenda kufuata elimu kijiji jirani.

Aveline Avitus ni mwanafunzi anayenufaika na uwepo wa shule ya sekondari Buzi amepongeza jitihada hizo na kueleza kwamba kabla ya vyumba hivyo vya madarasa ambapo Serikali ilijenga viwili na umoja umejenga vitatu,wazazi walilazimika kuamka saa 11.00 alfajiri  kuwapeleka watoto wao shuleni katika kijiji kingine kwa kuofia watoto wao wanaweza kudhulika na wanyama wakali kutoka na uwepo wa tingatinga ambalo utunza wanyama aina ya viboko.

Kadhalika kupitia maadhimisho hayo wanabuzi wamefanya halambee ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya Kijiji kwa kukusanya shilingi Milioni 8 huku Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya awali na Msingi Rweikiza  ambaye alimwakilisha  wa Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Jasson Rwekiza yeye akachangia kiasi cha shl mil. tatu iliyotolewa na mbunge huyo.











Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top