UDSM Yaanzisha Programu ya Mafunzo ya Nyukilia kwa Matibabu na Kujenga Uwezo wa Taifa

0


Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeanzisha Programu Maalumu ya Mafunzo ya Nyuklia katika Masuala ya Matibabu, ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha uwezo wa kitaifa wa kutoa huduma za afya zinazotegemea teknolojia ya kisasa ya nyuklia.

Akizungumza Septemba 25, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa programu hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema kuwa Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika ununuzi wa vifaa na mitambo ya matibabu ya kisasa katika hospitali mbalimbali nchini. 

Hata hivyo, idadi ya wataalamu waliopo ni ndogo, hivyo kuna uhitaji wa dharura wa kuongeza wataalamu wa ndani wenye ujuzi wa kutumia teknolojia hiyo.

Prof. Nombo alieleza kuwa kutokana na changamoto hiyo, Wizara iliielekeza UDSM kuandaa programu hiyo maalumu ili kuwezesha nchi kuandaa wataalamu wa nyuklia kwa matibabu ndani ya nchi, badala ya kutegemea mafunzo kutoka nje.

 Programu hiyo itatolewa katika ngazi ya shahada ya kwanza na shahada ya pili, na wahitimu wake watafanya kazi katika vituo vya afya na hospitali mbalimbali nchini.

Aidha, Prof. Nombo alibainisha kuwa programu hiyo itakuwa ya kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki, na hivyo kuvutia wanafunzi kutoka nchi jirani kuja kusoma nchini Tanzania. Hii ni fursa ya kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha elimu ya nyuklia kwa matibabu katika eneo hilo.

Programu hii imeandaliwa kwa ushirikiano na Tume ya Nguvu za Atomiki pamoja na Taasisi ya Kimataifa ya Masuala ya Nyuklia. Tayari shahada ya kwanza imedahili wanafunzi 20 waliokidhi vigezo, huku shahada ya pili ikiendelea na udahili ambapo hadi sasa wanafunzi saba wameshaandikishwa.

 Hatua hii ni ya kihistoria katika kuimarisha rasilimali watu wa ndani na kuhakikisha matumizi salama na sahihi ya teknolojia ya nyuklia katika sekta ya afya.

Chanzo: wizara ya elimu sayansi na teknolojia







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top