Watumishi wa umma watakiwa kujiandaa na mabadiliko ya teknolojia

0

Na Ghati Msamba.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, amewataka watumishi wa umma nchini kujipanga na kuendana na mabadiliko ya teknolojia, hususan matumizi ya Akili Unde (Artificial Intelligence – AI), ili kuimarisha usimamizi na maendeleo ya rasilimali watu katika utumishi wa umma.

Waziri Kikwete ametoa wito huo Novemba 10, 2026, aliposhiriki ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Tawala na Rasilimali Watu Afrika uliofunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika Hoteli ya Verde, Zanzibar.

Amesema mabadiliko ya teknolojia yanayoendelea kushika kasi duniani yanapaswa kuchukuliwa kama fursa na chachu ya kuboresha utendaji kazi, kuimarisha mifumo ya usimamizi wa rasilimali watu pamoja na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Aidha, amewahimiza watumishi wa umma kutambua umuhimu wa kujiendeleza kitaaluma na kujenga uwezo wa kutumia teknolojia mpya ili kukabiliana na changamoto na kutumia fursa zinazotokana na mabadiliko hayo.

Mkutano huo umehudhuriwa na washiriki takribani 1,220, wakiwemo Maafisa Tawala na Rasilimali Watu kutoka maeneo mbalimbali barani Afrika, ukiwa na lengo la kujadili nafasi ya utumishi wa umma na ulinzi wa rasilimali watu katika kipindi hiki cha mabadiliko makubwa ya kiteknolojia, hususan matumizi ya Akili Unde.

Mkutano huo unatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu, maarifa na mikakati itakayosaidia kuimarisha usimamizi wa rasilimali watu na kuendeleza utumishi wa umma unaoendana na mahitaji ya sasa na ya baadaye.






Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top