Muleba : Wazazi wametakiwa kuwaruhusu watoto na vijana wao kushiriki katika michezo kwani huwajengea Afya bora,kuwapatia ajira na kuwaepusha kuingia katika janga la matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
Wito huo umetolewa na Afisa mnadhimu mkoa wa Kagera kamishna msaidizi wa polisi (ACP) Yussuf Daniel wakati akimwakilisha kamanda wa polisi wa mkoa huo Blasius Chatanda katika fainali za Mwijage CUP yaliyofanyika Kamachumu Wilaya ya Muleba mbapo,amemshauri mkurugenzi na mwandaaji wa mashindano ya Paul Mwijage Cup kuanzisha pia timu za vijana chini ya miaka 17 ili kuibua vipaji halisi vinavyopatika Kamachumu.
"Mitandao ya kijamii wengi wetu wananchi tunaitumia vibaya,pale tunapoitumia vibaya inaleta athari kubwa kwa kijana mmoja mmoja,kwa wale wa Kamachumu lakini pia kwa jamii yetu yote kwa ujumla hivyo, ni vyema kujiepusha na ombwe hilo ili tubaki salama"amesema Yussufu
Pia amemshauri mkurugenzi wa mashindano hayo kuanzisha timu ya vijana wadogo ili kupata vipaji halisi kuanzia ngazi ya chini.
Naye mkurugenzi wa mashindano hayo Paul Mwijage alisema yanalenga kuinua vipaji vya vijana wa kamachumu na watakaofuzu mashindano haya watapatiwa nafasi ya kushiriki katika michuano mikubwa katika timu mbalimbali ikiwemo Kagera Sugar na Geita gold.
Mwijage ameongeza kuwa wataunda uongozi na katiba kupata timu ya kamachumu FC ambayo itakua ni timu ya wananchi ambayo wanatarajia kuipambania ili ishiriki lingi kuu Tanzania Bara.
Kwa upande wa katibu wa itikadi,uenezi na mafunzo wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kagera Hamimu Mahmudu amewashukuru waandaji wa mashinda ya Paul Mwijage CUP kuibua fursa ya ajira na kukuza vipaji vya vijana ili kupata wachezaji wakubwa kutoka kamachumu kama vile walivyopatikana Salum Ahmed Harufani, Adala Ahmedi Harufani, Wile Kamugisha na Didas Zimbiile.
![]() |











