Serikali Kuendelea Kutenga Fedha za Mendeleo Endelevu kwa Taifa - Mhe. Nanauka

0


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka amesema kuwa serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu, kuboresha huduma za kijamii na kufanya uwezeshaji kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Mhe. Nanauka amesema hayo  Julai 23 wakati wa mkutano wa hadhara aliofanya katika Kijiji cha Ikulwe ambako amehitimishia ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.

Ameongeza kuwa, katika kuhakikisha maendeleo endelevu ya taifa, serikali itaendelea kuboresha sera za uchumi wa nchi ili kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shuguli za uzalishaji mali na kuchangia uchumi wa taifa ili waweze kuwa wamiliki wa uchumi huo.

"Serikali itaendelea kufanyia kazi uwezeshaji wa wananchi wenye biashara changa, na bishara dogondogo ili washiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji zitakazowaletea maendeleo na kuwafanya kuwa wamiliki wa uchumi  wa taifa letu." 

Mkutano huo umeenda sambamba na tukio la Waziri Nanauka kukabidhi mfano wa hundi ya milioni 361.3 ikiwa ni mkopo wa asilimia kumi utakaonufaisha vikundi vya vijana, wanawake na walemavu.

Isack Charles ambaye ni mmoja wa vijana ambao ni wanufaika wa mikopo hiyo, ametoa rai ya mikopo hiyo kutolewa kwa wakati ili viweze kukuza mitaji yao na kupanua shughuli za uzalishaji.

✍️maendeleo ya vijana



Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top