Na WMJJWM Rome Italia
Tanzania imeendelea kuonesha dhamira yake ya kuimarisha usawa wa kijinsia, amani na usalama kwa kushiriki katika Mkutano wa Nane wa Ngazi ya Juu wa Mtandao wa Kimataifa wa Nchi zinazotekeleza Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama (WPS) uliofanyika jijini Rome, Italia, Juni 8 hadi 10, 2026.
Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Jinsia na Wanawake kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu.
Mkutano huo ambao umeandaliwa na Sekretarieti ya Mtandao wa Kimataifa wa WPS chini ya UN Women kwa ushirikiano na nchi ya Italia na Ufilipino ambazo kwa mwaka 2026 zilikuwa zikihudumu kama Mwenyekiti na Mwenyekiti Mwenza wa mtandao huo umewakutanisha wawakilishi kutoka nchi zaidi 70 duniani, ulijadili mustakabali wa ajenda ya wanawake katika masuala ya amani na usalama.
Miongoni mwa mambo ya kipaumbele ni utekelezaji wa Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama katika kukabiliana na changamoto zinazoendelea za amani na usalama duniani. Washiriki walisisitiza umuhimu wa kuweka mkakati madhubuti unaozingatia matokeo ili kuhakikisha malengo ya ajenda hiyo yanafikiwa kwa ufanisi.
Aidha, mkutano huo ulijadili umuhimu wa kuongeza ushiriki kamili, sawa na salama wa wanawake katika michakato ya kuzuia migogoro, kutatua migogoro na kujenga amani. Viongozi mbalimbali walikubaliana kuwa wanawake wana mchango mkubwa katika kujenga jamii zenye utulivu na maendeleo endelevu.
mkutano huo pia uliangazia changamoto mpya zinazohusiana na usalama, ikiwemo athari za mabadiliko ya tabianchi, uhamaji wa watu, maendeleo ya teknolojia za kidijitali pamoja na umuhimu wa kushirikisha vijana kupitia Ajenda ya Vijana, Amani na Usalama (YPS) ili kujenga kizazi chenye mchango chanya katika masuala ya amani.
Mazungumzo hayo yalijikita katika kuendeleza ajenda za maendeleo ya jamii, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake na makundi maalum pamoja na nafasi ya diplomasia katika kutangaza maslahi ya Tanzania kimataifa.
Mkutano huo umetoa fursa ya kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano utakaosaidia Tanzania kuendelea kunufaika
✍️maendeleo ya jamii


