Kampuni ya Zana za Kilmo Nchini ITALIA Yavutiwa Kuwekeza Tanzania

0


Kampuni ya SFOGGIA Iliyopo mji mdogo wa Padova, Jimbo la Veneto nchini Italia imevutiwa kuja kuwekeza nchini Tanzania ili kuonesha teknolojia walizonazo zenye kulenga kusaidia wakulima kuongeza tija katika uzalishaji, usalama wa chakula na lishe bora.

Katika ziara yake ya kikazi nchini Italia kutembelea Kampuni ya SFOGGIA tarehe 9 Juni 2026, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli amepokelewa na Mhe. Maria Bortoletto Mwakilishi wa Meya wa mji wa Montebelluna; Mhe. Maria Giovanna Favero, Makamu wa Meya mji wa Trevignano; Dkt Maria Teresa, Mmiliki wa Kampuni ya SFOGGIA; na Mwenyekiti wa kampuni hiyoB w. Antonio Sfoggia.

Katibu Mkuu Mweli ameambatana na Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk, Balozi wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwakilishi wa Kudumu katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Italia; Dkt. Yasinta Nzogela, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao; na Bi Jacqueine Mbuya, Mwambata Kilimo katika Ubalozi wa Tanzania nchini İtalya. 

SFOGGIA ni  Kampuni  ya Kiitaliano inayojihusisha na utengenezaji wa zana mbalimbali za kilimo hususan za kupandia mbegu za mazao ya nafaka, mbogamboga, mashine za kupanda miche (seed planter and seedling transplanter); pamoja na zana za kupalilia mazao (weeders).

Pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu Mweli amewaeleza kuhusu uwepo wa fursa za uwekezaji katika matumizi ya zana za kilimo nchini Tanzania na fursa ya soko na uwekezaji kwenye nchi zilizopo katika  jumuiya za SADC na EAC.

Matumizi ya zana bora za kilimo ni moja kati ya nyenzo muhimu ya kuchochea mageuzi katika Sekta ya Kilimo ambapo Serikali imekuwa ikifanya jitihada za kuboresha kusogeza mahitaji ya kilimo kwa mkulima kwa kuanzisha vituo vya zana za kilimo katika maeneo mbalimbali nchini ili  kuongeza tija na ubora wa mazao.

✍️wizara ya kilimo

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top