Mtambi Awataka Wananchi Mara Kutoa Taarifa za Viashiria vya Uhalifu na Uvunjifu wa Amani

0


Na Naziah Kombo, Mara.

WANANCHI mkoani Mara wametakiwa kutoa taarifa kwa vyombo husika kuhusu viashiria vya uhalifu au dalili zozote za vitendo vinavyoweza kuvuruga amani na usalama katika maeneo yao kwa wakati kabla havijaleta madhara kwa jamii.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya dola katika kudumisha usalama.

Kanali Mtambi alisema kumekuwa na taarifa za uvumi na mikusanyiko isiyo rasmi inayoweza kuchochea taharuki au kuhatarisha utulivu wa wananchi ikiwa haitafuatiliwa kwa karibu.

Alieleza kuwa utoaji wa taarifa kwa wakati ni njia muhimu ya kuzuia matukio ya uhalifu na uvunjifu wa amani kabla hayajatokea.

Aidha, aliwataka viongozi wa vijiji na mitaa kuwa mstari wa mbele katika kufuatilia mwenendo wa watu wanaoishi katika maeneo yao pamoja na wageni wanaoingia na kutoka, ili kubaini mapema vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa jamii.

Aliongeza kuwa amani na usalama ni jukumu la kila mwananchi, hivyo ushirikiano na utoaji wa taarifa sahihi kwa mamlaka husika ni muhimu katika kuimarisha utulivu na maendeleo ya jamii.

“Ni wajibu wa kila kiongozi wa serikali ya kijiji au mtaa kufuatilia mienendo ya wananchi wake na wageni wanaowasili katika maeneo yao, hatua hii itasaidia kubaini viashiria vya uhalifu na kuchukua hatua stahiki kwa wakati,” alisema Mtambi.







Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top