Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema inatarajia kuongeza idadi ya wataalamu wa kisasa katika sekta ya madini kupitia mafunzo yanayolenga kuinua ubora wa ufundi stadi nchini.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof. Adolf Mkenda, amesema wakufunzi 25 wanaoelekea nchini Finland wanapaswa kutumia vyema fursa hiyo ili kurejea na ujuzi utakaosaidia kukuza shughuli za uchimbaji na kuongeza thamani ya madini nchini.
Akizungumza Mei 5, 2026 jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwaaga wakufunzi hao, Prof. Mkenda amesema ujuzi watakaoupata utawezesha kuimarisha shughuli za madini na kuongeza ushindani wa madini ya Tanzania katika soko la kimataifa.
“Tunatarajia kupitia VETA, wataalamu wengi zaidi watazalishwa ili kusaidia kuongeza thamani ya madini yetu nendeni mkafungue macho, mjifunze teknolojia mpya na mbinu bora zitakazokuwa na tija kwa Watanzania,” amesema Prof. Mkenda.
✍️wizara ya elimu,sayansi na teknolojia








