Tanzania Kinara Afrika Katika Mageuzi ya Kodi - AFDB

0


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan, ameshiriki Mkutano wa 61 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) unaoendelea Brazzaville, Congo, ambapo Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi kinara Afrika katika mageuzi ya kodi, usimamizi wa fedha za umma na matumizi ya mapato ya ndani kugharamia maendeleo.

Hayo yalielezwa wakati wa uzinduzi wa taarifa ya African Economic Outlook 2026, ambapo Dkt. Mwigulu alishiriki mdahalo maalum kuhusu uzoefu wa Tanzania katika usimamizi wa uchumi.

Akizungumza kwenye mdahalo huo, Dkt. Mwigulu alisema Tanzania imefanikiwa kugharamia zaidi ya asilimia 70 ya bajeti ya Serikali kwa kutumia mapato ya ndani kupitia maboresho ya mifumo ya kodi, matumizi ya teknolojia za kidijitali na kuimarisha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma.

Alisema mafanikio hayo yamewezesha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kwa fedha za ndani ikiwemo Bwawa la Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dodoma na Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Katika mkutano huo, viongozi wa Afrika walisisitiza umuhimu wa nchi za bara hilo kutumia rasilimali za ndani, mifuko ya hifadhi ya jamii, sekta ya bima na mageuzi ya kisera ili kuimarisha uchumi na kupunguza utegemezi wa misaada ya nje.








Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top