Watoto Wanne Wafariki Dunia Bukoba Baada ya Kuangukiwa na Ukuta

0




Na Angela Sebastian 

Bukoba : Watoto wanne wa familia mbili wa mtaa wa Anyama kata ya Kibeta Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa Parfect Hoteli iliyoko jirani na nyumba mbili walimokuwa wakiishi kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo.


Kwa mujibu wa taarifa ya  Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Bukoba, Mkoa wa Kagera, Charles Kahigi alisema kati ya saa 12 hadi saa moja leo asubuhi walipokea miili ya watoto hao ambao kwa sasa ni marehemu ambapo, alitaja majina yao kuwa ni Maniath Ally miaka minne na Nunihani Ally  (10) wote wa kike wa familia ya Mickdad Ally.

Aliwataja wengine kuwa ni Elizabeth Edmund (12) wa kike na Edwin (10) watoto wa familia ya Edimund Matungwa wote wa mtaa huo.

Alisema uchunguzi umeishakamilika imebainika kuwa walikosa hewa kutokana na kifusi cha mchanga wa ukuta huo ambao ulikutwa umeziba maeneo ya pua lakini miili yao haikuwa na majeraha.

Edina Byera ni jirani wa familia hizo ambaye pia ni shuhuda wa tukio hilo amesema saa 11.30 alfajiri wakati mvua ikiendelea kunyesha alisikia kelele za kuomba msaada ndipo alikimbia akielekea eneo la tukio ambapo alikuta ukuta umeishaporomoka huku wananchi wakifanikiwa  kuokoa miili ya watoto watatu huku,wakiendelea kutafuta wa nne. 

Kaimu kamanda Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kagera Joseph Ngonyani alisema  walipata taarifa ya tukio la kuanguka kwa ukuta wa uzio wa Hoteli ya Parfect na kufika eneo la tukio saa 12.20 ambapo saa 12 50 walikuta  wananchi waliishanza kufanya maokozi na kuokoa watoto watatu kisha wakaungana nao na kuokoa mwili wa mtoto  mmoja ambaye uliokuwa umebakia na kisha kupeleka miili hiyo Hospitali ya rufaa

Alisema chanzo cha tukio hilo ilibainika kuwa ukuta huo uliloa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku  na na kumeguka ndipo ukaporomokea nyumba zilizoko jirani na kusababisha ajali hiyo.

Aidha Ngonyani aliwashauri wananchi kuchukua tahadhari zaidi hasa katika kipindi hiki cha mvua kubwa, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha majengo yao yako imara ili kuepusha madhara kama hayo.









Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top