Uzalishaji wa Mazao Asilia ya Biashara Nchini Waendelea Kuimarika

0

Uzalishaji wa mazao asilia ya biashara nchini umeendelea kuimarika, ukifikia tani 1,599,945.66 katika mwaka wa kilimo 2025/2026, sawa na asilimia 71.9. Hii ni ongezeko la asilimia 10.0 ikilinganishwa na tani 1,451,694.11 zilizozalishwa katika mwaka 2024/2025.

Takwimu hizo zimewasilishwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb), wakati akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa Fedha 2026/2027 tarehe 28 Aprili 2026, jijini Dodoma.

Mhe. Chongolo ameeleza kuwa uzalishaji wa mazao mbalimbali umeonesha mwelekeo chanya, ambapo zao la korosho limeongoza kwa kufikia tani 617,683.77, zao la pamba limezalisha tani 222,014, huku pareto ikifikia tani 2,780.

Aidha, uzalishaji wa kahawa umefikia tani 74,663.60, tumbaku tani 185,776, na chai tani 11,631.48. Kwa upande wa mazao mengine, mkonge umezalishwa kwa tani 64,321.77, sukari tani 410,979.04, na kakao tani 10,096.

Akiwasilisha kuhusu Mpango wa kuendelea kukuza uzalishaji wa mazao hayo, Mhe. Chongolo amesema Wizara imepanga kuongeza uzalishaji kutoka tani 1,599,945.66 mwaka 2025/2026 hadi tani 2,118,000 mwaka 2026/2027.

✍️wizara ya kilimo

 

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top