Askofu Malasusa Azipongeza Taasisi za Kemebos na Kaizirege

0

Na Angela Sebastian 

Bukoba:  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Alex Malasusa, amepongeza juhudi na uwekezaji mkubwa wa kisasa uliofanywa na taasisi za elimu za Kemebos na Kaizirege, akisema kuwa ni hatua nzuri inayosaidia kuleta maendeleo ya vijana na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa hafla za kuhitimu kidato cha sita mwaka 2026 zilizofanyika katika viwanja vya shule hizo, Askofu Malasusa alisisitiza umuhimu wa umoja, amani, hekima, na elimu bora kwa ustawi wa jamii. 

Alisema kuwa kutokana na uwekezaji huo mzuri ,hana budi kukili kuwa yeye pamoja na viongozi wa Kanisa hilo wataendelea kuitangaza shule hiyo uku wakieleza ufaulu mzuri wa wanafunzi wanaohitimu masomo yao katika shule za Kemiboss na Keizirege .

Askofu Malasusa alieleza kuwa, “Wimbo wa Taifa unapoimbwa unakaa kama sala au maombi kwa Mungu, ambapo tunaomba Afrika na Tanzania iwe na umoja, amani na hekima. Hii ni ndoto ya kila Mtanzania, na ni jukumu letu sote kuhakikisha tunaiendeleza.

 Aidha, alisisitiza kuwa, “Hekima inapatikana katika malezi bora yanayojumuisha wazazi wote wawili na katika shule zinazotoa elimu ya hali ya juu kama Kemebos na Kaizirege. 

"Tukiwa na umoja wa familia na jamii, tunaweza kuleta mabadiliko chanya kwa vijana wetu,tukiona matokeo yasiyo mazuri katika jamii, tujiulize kama wazazi tumefanya sehemu yetu sawasawa. Kama wimbo wa Taifa unasema, tunaomba Mungu atuletee umoja na kutojenga kebehi miongoni mwa watu wetu.”alisema Malasusa

Akiwaasa viongozi wa dini na serikali, askofu alisisitiza kuwa, “Ni wakati wa kujadili na kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha watu wanapata elimu ya kumjua Mungu na kuendesha nchi kwa maadili na viapo vinavyostahili. 

"Viongozi wa dini wanapaswa kuleta mwelekeo wa kujenga taifa lenye amani, hekima, na umoja,Viongozi wa dini wanajua maana ya amani, hivyo kila mmoja anapaswa kuombea amani kwa pamoja na tuwaunge mkono wahubiri wa amani na kuwatia moyo, huku tukikataa wanaovunja amani yetu.”aliongeza

Akizungumza kuhusu wanafunzi watakaohitimu, Askofu Malasusa aliwataka wahitimu kuwa makini na elimu yao, akisema Elimu ni uzima wao na ni msingi wa mafanikio yao ya baadaye,Wazazi wanapaswa kuendelea kuwasaidi watoto wao kwa malezi bora, kwani safari ya elimu inaanza sasa na itakuwa na manufaa makubwa kwa mustakabali wa Taifa letu.

 Kwa upande wake, Mkuu wa shule za Kemebos na Kaizirege, Kisha Ilamulila, alieleza kuwa, “Wanafunzi 212 wanatarajiwa kuhitimu kidato cha sita mwaka huu, ikiwa ni mafanikio makubwa kwa shule hizi. Tunatoa wito kwa wanafunzi kujiandaa kwa mtihani wa kitaifa utakaofanyika Mei nne, mwaka huu.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera, alihakikisha kuwa serikali inathamini mchango wa shule hizo katika kuendeleza mkoa wa Kagera kitaifa, akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kufikia malengo ya elimu na maendeleo. 





 

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top