Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini, Mhe. Balozi Chen Mingjian katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje jijini Dar es Salaam, Tanzania, tarehe 14 Aprili 2026.
Mazungumzo hayo yamelenga kuendelea kuimarisha ushirikiano imara na wa kihistoria uliopo baina ya nchi zetu
Dkt. Shelukindo, ameishukuru Serikali ya China kuendelea kuwa mshirika muhimu katika juhudi za kuleta maendeleo hususani kupitia miradi ya ushirikiano chini ya jukwaa la FOCAC.
Katika kuhamasisha ushirikiano wa raia wa nchi zetu hizi mbili na kurahisisha shughuli za wananchi hatua mbalimbali zimejadiliwa na namna ya utekelezeji wake Kwalengo la kurahisisha uhusiano na mawasiliano Kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili. (people to people exchanges)
Kwa upande wake Mhe. Balozi Chen Mingjian ameeleza kwamba China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha ushirikiano kupitia sekta mbalimbali ikiwemo za maji, kilimo, afya, umeme na miundombinu itakayochangia katika maendeleo endelevu na na kuboresha maisha ya wananchi wa nchi zetu hizi mbili.
✍️wizara ya mambo ya nje






