ICCAO Tanzania Yafanya Utafiti wa Matumizi ya Pombe na Athari zake Mkoa wa Mara

0


 Na Emmanuel Chibasa.

Wakati Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) ikitangaza kuwa ipo mbioni kuleta dawa ya kuacha pombe ili kuweza kusaidia kundi la watu wenye changamoto ya uraibu huo, Utafiti wa msingi wa mradi wa Ulevi Sio Dili uliofanywa na shirika la Intergrating Capacity and Community Advancement Organisation (ICCAO) mwaka 2026 katika Mkoa wa Mara, umebaini hali ya matumizi ya pombe na athari zake katika jamii.

Kwa mujibu wa ripoti ya ( Baseline Survey for the Ulevi Sio Dili Project in Mara Region) iliyotolewa February 2026, inaonyesha utafiti ulihusisha washiriki 337 kutoka wilaya za Musoma, Bunda na Butiama kupitia dodoso na makundi lengwa ili kuchunguza kiwango cha matumizi ya pombe, sababu zake na madhara yake ambapo matokeo yanaonyesha kuwa pombe inaathiri familia, vijana na watoto kupitia ukatili na umasikini. Hivyo, utafiti huu unaweka msingi wa hatua za kupunguza athari za pombe katika kipindi cha mradi wa 2026–2028.

Utafiti huo unaonyesha sababu kuu zinazopelekea matumizi ya pombe ni pamoja na starehe (59%), msongo wa mawazo (19%) pamoja na ushawishi wa marafiki pamoja na wazazi huku wilaya za Butiama na Bunda zikiwa zinaongoza kwa kiwango kikubwa cha matumizi ya pombe ukilinganisha na Musoma Manispaa na Musoma Vijijini.

Butiama imeonyesha viwango vya juu zaidi kutokana na wingi wa vituo vya uuzaji na uzalishaji wa pombe za kienyeji pamoja na urahisi wa upatikanaji. Bunda nayo inaonekana kuwa na changamoto kubwa inayochochewa na matumizi ya pombe miongoni mwa wanaume na vijana pamoja na athari za kiuchumi kwenye familia. Hali hii inaweka Musoma katika nafasi ya chini kidogo ingawa bado ipo kwenye hatari ya kuongezeka kwa tatizo hilo.

Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 49.5 ya watumiaji waliathiriwa na marafiki kuanza kunywa  huku 21% wakieleza kuwa walishawishiwa na wazazi au walezi wao. Mbali na hilo, utafiti umeonyesha uwepo mkubwa wa pombe katika jamii ambapo kwa wastani kuna vituo sita vya kuuza pombe katika kila kijiji na wazalishaji wanne wa pombe za kienyeji hali inayorahisisha upatikanaji wake kwa asilimia 79.2 ya wananchi.

Athari za matumizi ya pombe zimeonekana kuwa kubwa katika jamii ambapo asilimia 34.7 ya washiriki walikiri kufanyiwa ukatili na mtu aliyekuwa amelewa, huku asilimia 12.2 wakisema walifanyiwa ukatili na wazazi au walezi waliokuwa chini ya ushawishi wa pombe. Pia, asilimia 11 waliripoti kukosa mahitaji muhimu kutokana na wazazi kutumia kipato kwenye pombe.

 Licha ya uelewa mkubwa kuhusu madhara ya pombe kwa afya (zaidi ya asilimia 97), bado matumizi yanaendelea, jambo linaloonyesha hitaji la hatua madhubuti zaidi za elimu, udhibiti na utekelezaji wa sheria ili kupunguza athari hizi katika jamii.

April 24, 2026 meneja  wa MSD Kanda ya Dodoma, Mwanashehe Jumaa akizingumza wakati wa mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kusuhu utekelezaji wa majukumu ya MSD, alisema kuwa wako mbioni kuleta dawa ya kuacha pombe ili kusaidia kundi la watu wenye changamoto za urahibu huo.

Amesema kwa muda mrefu dawa hizo zilipatikana katika baadhi ya famasi lakini kwa sasa MSD kwa kushirikiana na Mirembe wataanza wataanza kuziingiza dawa hizo nchini.

“ Hapo awali ilikua ni vigumu sana kwa mgonjwa kuandikiwa dawa hizi, sasa tumeipata dawa hii kwa gharama nafuu na itasambazwa na dawa hizi zinatibu uraibu wa pombe na si sigara” Amesema Mwanashehe

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top