Watu wenye ulemavu wa macho Bukoba waiomba BoT kutoa elimu ya utambuzi wa noti

0


 Na Angela Sebastian 

Bukoba  : WATU wenye ulemavu wa macho (wasioona) mkoani Kagera wameiomba Serikali kupitia Banki Kuu ya Tanzania (BoT) kutoa elimu ya utambuzi wa noti ili nao waweze kwendana na wakati huu wa sayansi na teknologia kwasababu  wanatambua fedha hiyo kutokana na hisia na  uzoefu.

Mwalimu mstaafu Analise Rubago ni mwenyekiti wa chama cha wasioona  mkoa wa Kagera akiongea leo na mwandishi wa habari hii katika ofisi za chama hicho mkoani humo,ambapo amesema hakuna alama zinazotambulisha noti halisi kwahiyo ziwekwe zijulikane ili waweze kuzisoma  maana wao wanasoma kwa kutumia vidole.

"Niliwahi kusikia BoT wanatangaza kuwa kuna utambuzi wa noti kwa watu wasioona nafikiri ilifanyika Kitaifa yaani Tanzania nzima lakini mimi sijui kwenye noti kama kuna alama yoyote ya utambuzi,ambayo mtu asiyeona anaweza kuitambua kwa kuigusa kama tunavyogusa vitabu vya nukta nundu,mfano ni hii hapa noti nimeishika naitambua kuwa ni 10,000 kutokana na uzoefu wa upana na urefu kwamba maana elfu kumi ni ndefu pia ni kubwa lakini 1000 ni ndogo na fupi"ameeleza Rubago

"Kwahiyo tunaishauri BoT kutupatia elimu ya utambuzi kama kuna alama ambazo zipo kwenye noti au waweke nukta fulani pembeni inayotambulisha hii ni noti ya kiasi fulani na siyo bandia lakini sasa tunazitambua kwa urefu na upana hivyo,ata noti bandi sisi siyo rahisi kuzigundua ila  tukipata elimu tutaepukana na adha hiyo na kutuweka salama zaidi na kuendana na sayansi na teknolojia ya sasa"ameeleza Rubago

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top