Rhobi Samwelly : Usalama wa watoto ni jukumu la kila mtu

0


Mwandishi Wetu, Musoma.

Imebainishwa kuwa,  jukumu la kuhakikisha usalama wa watoto si la mtu mmoja, bali ni dhamana ya kila mtu  kushiriki kikamilifu kuona kwamba, watoto wanalelewa katika mazingira  salama na bora. 

Akizungumza na Musoma News Hub, Mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania linalopambana na ukatili  Mkoa wa Mara, Rhobi Samwelly, amesema watoto ni hazina ya taifa inayohitaji ulinzi wa pamoja. Huku akisema kila mwana Jamii atambue  wanapaswa kuishi bila hofu ili waweze kukua na kutimiza ndoto zao.

Rhobi amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji huacha majeraha ya kudumu kwa watoto. Ameonya kuwa,  kimya cha jamii huwapa nguvu wanaofanya ukatili kuendelea na vitendo vyao, hivyo akasisitiza umuhimu wa kuripoti matukio ya ukatili Katika vyombo vya  sheria. 

Aidha,  amesema  vyombo vya habari na mashirika yasiyo ya kiserikali  mchango wao ni  mkubwa katika kuhamasisha jamii kushiriki katika mapambano ya ukatili wa Kijinsia. Ambapo   ameomba  ushirikiano uendelee kuwepo kati ya serikali, taasisi mbalimbali  na wananchi katika kusaidia  usalama wa watoto kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top