Je unatumia SHISHA? Fahamu Madhara yake kwa Binadamu

0


Katika miaka ya hivi karibuni, matumizi ya shisha yameongezeka kwa kasi miongoni mwa vijana katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania, hasa katika miji na maeneo ya burudani. Wengi wamevutiwa na mtindo huu wakiamini ni njia ya kujiburudisha au kupunguza msongo wa mawazo, bila kufahamu hatari kubwa zinazoweza kujificha nyuma ya moshi huo.

Kwa mujibu wa shirika la ICCAO Tanzania matumizi ya Shisha si salama kama baadhi ya watu wanavyodhani. Moshi wake una kemikali hatarishi zinazoweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya binadamu na hata kwa watu wanaokaa karibu na wanaovuta. Ni muhimu jamii, hasa vijana, kupata elimu sahihi kuhusu matumizi ya shisha na athari zake.

Shisha ni nini?

Shisha ni neno lenye asili ya misri lijulikanalo kama “sheesha” lenye maana ya bomba lililounganishwa kwenye chombo chenye maji linalotumika kuvutia tumbaku au aina nyingine ya kikevi kinachotumiwa kwa njia ya kuvuta.

Je ni yapi madhara ya matumizi ya tumbaku kwenye shisha? na haya ndio madhara ya kiafya kwa binadamu; 

👉 Inaelezwa kuwa uchangiaji wa matumizi husababisha kuambukizana maradhi kama vile kifua kikuu, fangasi na magonjwa mengine.

👉 Kemikali za tumbaku za kwenye shisha husababisha saratani ya mapafu, maradhi ya moyo na maradhi ya mfumo wa njia ya hewa.

👉 Nikotini inayotokana na tumbaku kwenye shisha huongeza kasi ya mapigo ya moyo na shinikizo la damu.

👉 Kuzaliwa kwa watoto wenye uzito mdogo, ugumba kwa wanaume, magonjwa ya moyo, fizi, pua na maradhi ya akili.

👉 Saratani ya mapafu, kibofu cha mkojo, tumbo, kinywa na koromeo.

👉 Mkaa unatumika kuzalisha hewa ya kaboni monoksaidi ambayo ni sumu inayoweza kusababisha kifo ikiwa itavutwa kwa kiasi kikubwa.

👉 Watu wanaokaa karibu na watumiaji wa shisha huathirika kwa kuvuta hewa ya kabonimonoksaidi na taka zingine ambazo huzalishwa kwa wingi kuliko zinazozalishwa kwenye moshi wa sigara ya kawaida.

👉 Kuna tabia ya kuchanganya heroin au bangi au vyote kwa pamoja kwenye tumbaku inayotumika huku watumiaji wakijua au kutojua hivyo kujikuta wanakuwa wategemezi wa dawa hizi.

👉 Nikotini iliyo kwenye tumbaku ya shisha huleta hali ya uraibu.

Elimu hii ya madhara ya matumizi ya tumbaku kwenye shisha inaletwa kwenu na Shirika la ICCAO Tanzania kupitia mradi wake wa Ulevi Sio Dili kwa kushirikiana na Musoma News Hub.

✍️Imeandikwa na Emmanuel Chibasa

     Chanzo: ICCAO Tanzania


#UleviSioDili

#EpukaUleviLindaAfyaYako

#ICCAOTanzania

#MusomaNewsHub

#MusomaTv

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top