Fahamu kuhusu madhara ya Bangi Kwa binadamu na jamii

0



Kila kizazi kina vita yake. Kwa vijana wa leo moja ya vita kubwa siyo ukosefu wa fursa pekee, bali ni mtego wa dawa za kulevya unaonyemelea ndoto zao kimya kimya. Bangi, inayojulikana kwa majina kama msuba, ganja, blanti, kijiti au ndumu, mara nyingi huonekana kama kitu cha kawaida au cha kujiburudisha. Lakini nyuma ya moshi wake kuna madhara makubwa yanayoathiri ubongo, afya ya akili, mahusiano ya kifamilia na hata mustakabali wa taifa.

Wakati vijana wakidhani wanatafuta utulivu au kuondoa msongo wa mawazo lakini wataalam wa afya wanaeleza kuwa  bangi hubadilisha uhalisia, hupunguza uwezo wa kufikiri kwa makini na huweza kufungua mlango wa matatizo ya kiafya na kijamii yasiyorekebishika kirahisi na madhara mengine ni pamoja na;

·        1. Huamsha magonjwa ya afya ya akili

·        2. Kikohozi sugu, pumu, vidonda vya koo na saratani

·         3.Husababisha uraibu

·         4.Hupunguza uwezo wa kufikiri na kukumbuka

·         5.Kuona, kusikia na kuhisi vitu tofauti na uhalisia

·        6. Kuchochea uhalifu mfano wizi, utapeli na ukatili

·        7. Kupoteza nguvu kazi ya taifa

·        8. Huvuruga mahusiano ya kifamilia

·        9. Hupunguza ufanisi kazini na mashuleni

·        10. Husababisha matatizo ya uzazi

·        11. Kilimo cha bangi huharibu vyanzo vya maji, viumbe hai na uoto asilia

·        12. Kukosa mwamko wa maendeleo na kusababisha umasikini

Elimu hii ya madhara ya bangi kwa binadamu na jamii inaletwa kwenu na  shirika la ICCAO Tanzania kupitia mradi wa Ulevi Sio Dili, kwa kushirikiana na Musoma News Hub

Imeandikwa na Emmanuel Chibasa

Chanzo: ICCAO Tanzania

#UleviSioDili

#UleviSioDiliVijanaTuamke

#EpukeniUleviLindaAfyaYako

#ICCAO Tanzania

#MusomaNewsHub

 

 


Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top