TAKUKURU Kagera yabaini ukwepaji kodi na biashara za magendo Kyaka

0


 Na Angela Sebastian 

Bukoba : Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Kagera inaendelea kuwafuatilia watumishi wa  umma katika vituo vya ukaguzi mipakani wanaofumbia macho vitendo vya  ukwepaji kodi na upitishaji wa bidhaa kwa njia za magendo.

Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa taasisi hiyo Vangsada Mkalimoto baada ya Takukuru Wilaya Missenyi mkoani humo kwa kushirikiana na kikosi kazi cha kuzuia magendo kuakoa shilingi milioni 57.1 kutokana na kukamata, magari matano likiwemo lililobeba shehena ya pombe haramu, yakiwa yanavuka mpaka wa Tanzania na Uganda pamoja na vituo vya ukaguzi vya Kyaka bila kulipa kodi 

Akitoa taarifa ya mafanikio ya utendaji kazi  wa Takukuru kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba mwaka 2025 Mkalimoto leo, ofisini kwake mjini Bukoba alitaja magari hayo kuwa ni malori matatu yaliyobeba shehena ya karanga  tani 87 na kilogram 300 za maharage na hiace mbili moja ikibeba katoni 303 za pombe haramu na nyingine imebeba injini ya gari.

"Kutokana na operesheni yetu magari yaliyokamatwa na kupekuliwa ni Lori lenye namba T525 DNJ yenye trela namba T 811 DHA iliyobeba tani  38 za karanga kutoka Uganda, gari lenye namba T509 EDN(Fuso Tandam) iliyokuwa imebeba tani 16 na kilogram 300 za karanga na maharage kutoka Uganda na Lori lenye namba T457 ELV lenye trela namba T459 ELU lililobeba ta ni 33 za karanga kutoka Uganda" aliekeza Mkalimoto

Mengine ni namba T 754 DJW (Toyota Hiace) lililokuwa limebeba injini ya gari kutoka Uganda  na gari namba T 445 DFJ iliyokuwa limebeba pombe haramu katoni 303 kutoka Uganda ambapo magari hayo yote yamepatikana na kosa la uingizaji bidhaa nchini bila  kibali na kutokufuata taratibu zote za uigizwaji wa bidhaa nchini.

Alisema wamiliki wa magari hayo wamelipa faini za magari,mizigo na tozo za Serikali iliyotakiwa ambapo TAKUKURU inaendelea kuwafuatilia watumishi wa umma katika vituo vya ukaguzi wanaofumbia macho ukwepaji kodi na upitishwaji wa Magendo kuingizwa nchini.

Wakati huo huo TAKUKURU Wilaya ya Muleba imeokoa tofali 2,830 yenye thamani shl.mil.7.9 ambazo zingetumika katika mradi wa ujenzi wa jengo la mapokezi (OPD) katika kituo cha Afya cha kata Ngenge ambayo ilibainika kuwa chini ya kiwango cha ubora unaohitajika 



Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top