Wananchi Tumieni Huduma ya Umeme Kubadilisha na Kuboresha Maisha Yenu - Abdulrazack Mkomi

0


MKINGA : Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuthitibisha kwa vitendo nia yake ya kujali na kuthamini wananchi kwa kuhakikisha inafikisha huduma nafuu ya umeme kwenye kila kijiji na kitongoji mkoani Tanga ili huduma hiyo isaidie kubadilisha na kuboresha maisha ya wananchi mkoani humo.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa maendeleo ya jamii kutoka REA, ndugu Abdulrazack Mkomi wakati wa ziara ya uhamasishaji wananchi kujiunga na huduma ya umeme wilayani Mkinga mkoani Tanga.

Aidha Mkomi, amewasisitiza wananchi kuwa waangalifu wakati wa kufanya malipo ya kujiunga na huduma ya  umeme, akieleza kuwa gharama ya kuunganisha umeme vijijini ni shilingi 27,000 kwa  makazi na shilingi 139,000 kwa  Mitambo na mashine au viwanda na malipo yote yanalipwa kwa kutumia namba ya kumbukumbu inayotumwa moja kwa moja kutoka TANESCO  kwa njia ya meseji na si vinginevyo.

Aidha, uhamasishaji huo ulijikita zaidi katika kutoa elimu kwa wananchi ya namna ya kujiunga na huduma ya umeme na matumizi ya umeme yenye tija ikiwemo kuanzisha na kufanya  biashara kama saluni, uchomeaji, viwanda na nyengine nyingi ambazo zitasaidia kuongeza ajira na kipato.

Halikadhalika wananchi wameaswa kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa miundominu ya umeme ikiwemo nguzo, nyaya na miundombinu mingine ya umeme ili kuepuka uharibifu unaoweza kusababisha kukatika kwa huduma ya umeme pamoja na kuhatarisha usalama wa watu pamoja na mali.






Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top