Waamini wa Kanisa Katoliki Waanza Mfungo wa Kwaresima

0


 Na Robinson Wangaso Musoma. 

Waamini wa Kanisa  Katoliki kote duniani wameanza Mfungo wa Kwaresima leo Februari  18,  2026 Jumatano kwa kupakwa majivu katika paji la uso kama ishara ya toba na kukumbuka mates, kifo Na ufufuko wa Bwana Yesu Kristo.

Waamini wa Parokia ya Kristo Mfalme Rwamlimi Jimbo la Musoma wameshiriki adhimisho la misa takatifu iliyoanza saw 12.30 alfajiri na kuongozwa na Padre Joseph Sewangana ambaye pia ni Mkurugenzi wa shule ya Msingi BAKHITA ya Mjini Musoma. 

Padre Joseph amewakumbusha waamini hao kuwa Kwaresima ni kipindi cha kufunga, Katubu, kusali na kujitoa katika kuwasaidi wahitaji mbalimbali wa kimwili na Kiroho. 

Wakatoliki hufunga siku 40 kwa Maandalizi na majitayarisho kabla ya siku kuu ya Pasaka ambayo husherehekewa kote duniani kwa ukumbusho wa Ufufuko wa Kristo.

Hata hivyo padre huyo amewakumbusha waamini hao kwa kufunga ni pamoja ni kufunga matendo maovu na kuacha tabia zisizompendeza Mwenyezi Mungu. 

Amesisitiza na kurejea sheria za Kanisa Katoliki kuhusu kufunga chakula kwa wenye umri kuanzia miaka 14 na kuendelea huku Watoto Wadogo, wajazwazito Na wagonjwa wanaotumia dawa wakihimizwa kutofunga Chakula.



Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top