Seguda Ahukumiwa Kwenda Jela Miezi 14 Kwa Kosa la Kuua Bila Kukusudia Mtoto wake wa Miezi 9 Mwibagi

0


 Na Robinson Wangaso - Musoma 

Mahakama kuu kanda ya Musoma Mkoani Mara imemhukumu ndugu Saguda Sanga (35) mkazi wa kijiji cha Mwibagi Wilaya ya Butiama adhabu ya kwenda jela miezi 14 (Mwaka Mmoja na miezi 2) baada ya kupatikana na hatia ya kuuwa bila kukusudia mtoto wake Baraka Saguda mwenye umri wa miezi 9.

Hakumu hiyo imetolewa na Jaji Kamanzima Idd Kafanabo wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma Februari 2, 2026 katika Maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama kuu Kanda ya Musoma ambapo shauri hilo lilisikilizwa katika mahakama ya wazi na kufikia uamuzi wa papo hapo baada ya mtuhumiwa kukiri mbele ya mahakama kutenda kosa hilo.

Kwa mujibu wa Wakili wa Serikali mwandamizi ofisi ya Mashitaka Grace Madikenya ameieleza Mahakama Kuu kuwa mtuhumiwa alitenda tukio hilo Novemba 23, 2024 nyumbani kwake Mwibagi kwa kumpiga kwa bahati mbaya Mtoto wake huyo teke liliosababisha kifo akiwa analenga kumpiga Mkewe ambaye walikuwa katika mapigano, kwa bahati mbaya teke hilo likampiga mtoto Baraka ambaye alipoteza Maisha. Wakili huyo aliiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa mtuhumiwa na watu wengine wenye tabia na muenendo kama huo.

Baada ya kusomewa shitaka hilo, mtuhumiwa akiwa anatetelwa na wakili musomi Ostack Mligo akisaidiwa na Mwajuma Shaban waliiomba mahakama kuu kumpunguzia adhani kwani mtuhumiwa alitenda kosa hilo bila kukusudia huku akiwa kijana na baba wa familia ya wakeWawili na watoto tisa ambao wote wanamtegemea na ukizingatia amejuta kutenda kosa hilo na hakuweza kuisumbua mahakama. 

Baada ya mawasilisho ya pande zote, Jaji Kamanzima I. Kafanabo kwa kutumia kifungu cha 198 cha kanuni ya adhabu na kwa kuzingatia muda ambao mtuhumiwa mekuwa mahabasu tangu alipokamatwa Novemba 24, 2026 alimhukumu kwenda jela miezi 14 huku akisema ikiwa mtuhumiwa ama upande wa jamhuri hautaridhika na maamuzi unaruhusiwa kukata rufaa katika mahakama ya rufaa Tanzania. 


Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top