BoT yawashauri wananchi kutumia mifumo ya serikali kuwekeza katika dhamana

0


Na Angela Sebastian 

Kigoma : Mchambuzi kutoka kurugenzi ya masoko ya fedha wa Benki Kuu ya Tanzania  (BoT) Ephraim Madembwe, amewashauri wananchi kutumia mifumo ya Kiserikali kuwekeza katika dhamana za Serikali ili kunufaika na fursa za uwekezaji zenye usalama zaidi.

Ametoa wito huo leo  mkoani Kigoma wakati akitoa mada kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kagera,Kigoma, Katavi na Tabora walioko katika mafunzo ya siku mbili kwa lengo la kuwajengewa uwezo katika kuripoti  masuala ya uchumi na fedha kwa usahihi na weledi zaidi.i Pia kufahamu juu mabadiliko na utendaji wa shughuli mbalimbali za BoT.

 "Dhamana za Serikali zipo za aina mbili ambazo ni za muda mfupi na muda mrefu, na hupatikana kupitia mifumo rasmi ya Serikali ambayo ni  njia salama   inawawezesha wananchi na wawekezaji kupata faida huku, wakiisaidia Serikali kugharamia miradi ya maendeleo hivyo tunawashauri wazichangamkie maana ni fursa"ameeleza Madembwe 

Amesema uwekezaji huo unafanyika kupitia hati fungani ya Serikali kwa maana ya dhamana hizo za Serikali ambapo ni nyenzo kwani Serikali inazitumia kukopa kutoka kwenye soko hivyo, kupitia uwekezaji huo mwananchi anakuwa ameikopesha Serikali ambapo kuna faida ndani yake.

Amesema kuwa kwanza wataitumia kama dhama ya kupata mkopo kwa maana ya wawekezaji na wafanyabiashara pia kutumika kama kinga ya huo mkopo.

" Uwekezaji huo utashirikisha ata wakazi wa nchi za  Afrika Mashariki na  nchi za kusini mwa Afrika lengo tuwe na soko ambalo lina ukwasi wa kutosha"ameongeza 

Wakati  huo huo  Meneja Msaidizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki Kuu ya Tanzania,  Noves Moses,amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 14

tangu kuanza kwa programu ya mafunzo kwa waandishi wa habari, kumekuwa na ongezeko la utaalamu katika uandishi wa habari za uchumi, hali inayosaidia wananchi kupata taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu masuala ya fedha, matumizi bora ya pesa sambamba na sera za kifedha

Noves ameema kuwa kupitia vyombo vya habari, BoT imefanikiwa kufikisha elimu kwa umma kwa ufanisi zaidi, jambo linalochangia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya kifedha.

Meneja Msaidizi wa Uchumi na Takwimu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Shamy Chamicha, amewashauri wananchi kuwa na utaratibu mzuri wa utunzaji wa fedha husani noti ili ziweze kudumu kwa muda mrefu bila na kuchakaa.

Amesema kuwa inaonekana  baadhi ya noti, hususani za shilingi elfu moja na elfu mbili, zimechakaa kwa kasi kutokana na kutumika sana katika maeneo ya biashara zinazogusa jamii kwa kiasi kikubwa mfano wauzaji na wanunuzi wa mkaa .

Amesema kuwa utunzaji sahihi wa noti unasaidia kupunguza gharama za uchapishaji wa fedha mpya na kulinda ubora wa fedha zinazozunguka kwenye uchumi hivyo akawahimiza wananchi kuepuka kukunja, kuchana au kuandika juu ya noti, na badala yake watumie sehemu maalum kama vile pochi ili kuhifadhia fedha.







Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top