PSSSF Yawashauri Watumishi wa Umma Kutumia PSSSF PORTAL Kuhakiki Taarifa

0

Na Ghati Msamba-Musoma

Wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wameshauriwa kutumia mfumo wa kidijitali wa PSSSF Portal ili kupata na kuhakiki taarifa zao kwa haraka bila ulazima wa kufika ofisini.

Kauli hiyo imetolewa  na Kaimu Meneja   wa PSSSF mkoa wa Mara  Nuru Mahinya wakati akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya mfumo wa PSSSF Portal katika semina kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Mara  iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Adavi, mjini Musoma.

Mahinya amesema matumizi ya mfumo huo wa kidijitali yana faida kubwa kwa wanachama, ikiwemo uwezo wa kupata na kuhakiki taarifa za michango yao pamoja na historia ya michango kwa haraka na kwa urahisi, bila gharama na usumbufu wa kufika katika ofisi za PSSSF.


Kaimu Meneja PSSSF Mkoa wa Mara Nuru Mahinya Akitoa Mada kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara

Ameeleza kuwa mfumo wa PSSSF Portal ni salama zaidi ikilinganishwa na mifumo ya awali, hivyo amewahakikishia wanachama kutokuwa na wasiwasi wowote wanapotumia mfumo huo. Aidha, amesema kwa sasa wanachama wote wanalipa michango yao kwa wakati, jambo linalosaidia kuboresha utoaji wa huduma.

Akizungumza kuhusu mafao ya uzeeni, amesema mwanachama atakayeandaa mapema nyaraka na maombi yake ya ustafu, ataanza kupata pensheni yake ndani ya siku 14 baada ya kustaafu rasmi.

Vilevile, ameeleza kuhusu fao la ukosefu wa ajira, akisema mtumishi atakayepoteza ajira atalipwa fao hilo kwa kipindi cha miezi sita, ambapo atalipwa asilimia 33.3 ya mshahara wake wa msingi (basic salary) aliyokuwa anapokea.

Akijibu maswali na hoja zilizoulizwa na waandishi wa habari, amesema PSSSF imeendelea kuboresha mifumo na huduma zake ili kuhakikisha wanachama wanapata haki zao kwa wakati na kwa uwazi, huku akiwahimiza waandishi wa habari kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya mifumo ya kidijitali ya mfuko huo.


















 

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top