Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Ampongeza Rais Dkt. Samia

0


 Na Angela Sebastian 

Bukoba : Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Kagera Faris Buruhan  amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameendelea kuliongoza Taifa kwa uvumilivu na ustahimilivu, hata pale zinapotokea changamoto mbalimbali ameweza kuzitafutia ufumbuzi kwa hekima na busara.

Alisema hayo wakati wa Dua maalum aliyoiandaa mwenyekiti huyo kwa ajili ya kuliombea Taifa,Rais Dk.Samia na wasaidizi wake amayo imefanyika katika kata ya Katoro Bukoba vijijini na kuhudhuliwa na viongozi wa dini,Serikali,baadhi ya wabunge na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa na nje.

"Dk.Samia ameonyesha uongozi na ukomavu kwa kipindi cha miaka minne iliyopita na sasa baada ya uchaguzi wananchi ni mashahidi tumpe moyo,nguvu na kuendelea kusimama kumsemea pale wanapotokea wapotoshaji maana ushahidi upo hususani miradi mikubwa ya maendeleo iliyotekelezwa katika maeneo yetu"Faris

Alitoa mfano kwa shule aliyosomea ya Katoro sekondari kipindi "tunasoma tulikuwa na vyumba vitatu vya madarasa,walimu wawili na tukigombania viti kati ya walimu na wanafunzi aliyewahi ndo aliweza kukalia lakini leo shule ina vyumba vya kutosha,vifaa vya kutosha ikiwemo viti na meza,umeme na maji"

Aidha aliwashukuru wanachama wa CCM wa jimbo la Bukoba Vijijini walioshiriki katika kinyang'anyiro cha kura za maoni ndani ya chama hicho mwaka jana kwa kumpatia kura nyingi zipatazo 4,619 kwamba ni upendo na imani kubwa kwake hivyo ndiyo maana akaandaa Dua kumshukuru Mwenyezi Mungu na wananchi hao kwa ajili ya jambo hilo.

Pia alisema kwa umri wake kama kijana pia kiongozi wataendelea kulitumikia Taifa kwa kushirikiana na viongozi wenzake ili kumsaidia Dk.Samia kutatua changamoto za wananchi wa Kagera kupitia UVCCM kwani Mungu ana namna tatu za kuitikia dua kwanza anaweza kukupa moja kwa moja, ulkuchelewesha tatu unaweza kuomba hili akaupa lile hivyo kama hakupata ubunge Mungu atamjali wakati mwingine.

Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika dua hiyo alimpongeza Faris kwa kuandaa dua hiyo kwani ni jambo la kuigwa maana Taifa letu linapitia katika mapito pamoja na juhudi za wanadamu yote yanamtumainia sana Mwenyezi Mungu,kumuomba ulinzi ili nchi yetu iendelee kuwa salama,kusifika ndani na nje kuwa kisiwa cha amani duniani kote.

Shekhe Haruna Kichwabuta ni shekh wa mkoa wa Kagera aliwashauri wananchi wa mkoa huo kuendelea kudumisha amani na utulivu kama ilivyo jadi yao maana pasipo amani hakuna anayeweza kufanya jambo lolote lenye kuleta maendeleo. 

Shekhe Shabani Salehe Pembe ambaye ni Imam wa Masjid Mtambaji Kinondoni jijini Dar es Salaam ambaye alikuwa mgeni mharikwa alisema vijana wenye maono na kutenga muda wao ili kuandaa dua kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuomba kwa ajili ya Taifa na watu wengine hususani Viongozi ni wachache katika Taifa hili hivyo Farisi ni mfano wa kuigwa.

 Pembe aliiwaomba viongozi,wadau na wananchi kumtumia kijana huyo katika kuchapa kazi pale watakapoona inafaa kwasababu ni kijana wa mfano anayejituma ili wengine waweze kufanikiwa bila kubagua wala kujali kabira,dini wala itikadi za vyama ili hari aoneTaifa likisonga mbele.












Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top