Ziara hiyo imelenga kuboresha na kuharakisha utekelezaji wa miradi hiyo kabla ya kufunguliwa kwa shule.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meya Alex Nyabiti amesema lengo la ziara hiyo ni kuweka vipaumbele katika utekelezaji wa miradi ya elimu, sambamba na kuhakikisha watoto wanapata vyumba vya madarasa vya kutosha, ikizingatiwa kuwa shule zinatarajiwa kufunguliwa tarehe 13 Januari, 2026.
“Tutafanya vizuri endapo tutakuwa na ushirikiano wa pamoja, kuheshimiana katika utendaji wa kazi na kujipima katika nafasi tulizopewa. Hizi ni kazi za serikali, si za mtu binafsi,” amesema Meya Nyabiti.
Meya Nyabiti amesema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ilitoa fedha kiasi cha shilingi milioni 50 mwezi Aprili mwaka jana kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Makoko.
Hata hivyo, amesema ujenzi huo haujakamilika kutokana na uzembe wa baadhi ya viongozi kushindwa kusimamia mradi huo ipasavyo.
Kutokana na hali hiyo, Meya Nyabiti amemuagiza Mkuu wa Shule ya Msingi Makoko kufika ofisini kwake siku inayofuata kwa ajili ya kupewa maelekezo ya kikazi, akisisitiza kuwa endapo watashindwa kusimamia vyema mradi huo, shule hiyo haitapewa miradi mingine ya maendeleo.
Aidha, ameitaka Kamati ya Shule ya Msingi Makoko kusimamia kwa karibu ujenzi wa vyumba vinanavyojengwa




