Na Naziah Kombo-Bunda.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwalimu Hamis Samson Abdul, amerudisha rasmi fomu ya kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Bunda katika uchaguzi mkuu ujao.
Mwalimu Abdul amerejesha fomu hiyo Julai 1, 2025 kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Bunda, Bi. Evodia Edward, ambaye alimpongeza kwa hatua hiyo na kumtakia heri katika mchakato wa kuwania nafasi hiyo.
Hayo ameyasema mara baada ya kurejesha fomu, Mwalimu Abdul amesema kuwa dhamira yake ya kuwania ubunge ni kuendeleza juhudi za utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa vitendo, pamoja na kuhakikisha Jimbo la Bunda linasimamiwa kikamilifu bungeni ili liendelee kupatiwa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Aidha, Mwalimu Abdul ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa namna ambavyo serikali yake imeendelea kutoa fedha nyingi za maendeleo kwa maeneo mbalimbali nchini.
Anasisitiza kuwa lengo lake ni kuungana na Rais katika juhudi za kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na uzalendo.