Faris Buruhani Awaongoza Wanafunzi wa Shule ya Omumwani Kupanda Miti 2,000

0


 Na Angela Sebastian 

Bukoba : Mwenyekiti wa umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Kagera (UVCCM) Faris Buruhani amewaongoza  wanafunzi  650 wa shule ya sekondari  ya wasichana ya Omumwani iliyopo Manispaa ya Bukoba mkoani humo kupanda miti 2,000 kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Rais  Dk.Samia Suluhu Hassani.

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, Faris alisema kuwa lengo la tukio hilo ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia katika kulinda na kutunza mazingira, akisisitiza kuwa upandaji wa miti ni sehemu muhimu ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Alisema  kuwa jumuiya hiyo imeamua kuonyesha uzalendo wa vitendo kwa kushiriki katika shughuli zenye manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla ambapo wanafunzi wasichanawa shule hiyo wamekuwa sehemu ya kumbukumbu katika sherehe hiyo ya kuzaliwa kwa mwaka 2026.

Alisema  kuwa vijana wa mkoa wa Kagera wanamuunga mkono Rais na wanampongeza kwa kazi nyingi anazofanga ikiwemo kudumisha amani,mshikamano ,uongozi bora  na kusimamia kwa weledi miradi mingi inayogusa wananchi wote.

Amesema wamechagua shule hiyo ya wasichana kama sehemu ya  kuwatia moyo  wa  kutumiza  ndoto  zao katika masomo na Kupata nyadhifa mbalimbali za kuwatumikia wananchi  katika siku zijazo ambapo amewashauri wanafunzi hao kulinda miti iliyopandwa na kuhifadhi mazingira sambamba na kuendelea kumuombea Dk.Samia ili aendelee kufanya kazi zake kwa weledi na uaminifu.

Zoezi hilo la kupanda miti katika shule hiyo limeshirikisha wasichana 650, wa shule hiyo walimu na vijana kutoka kata  mbalimbali za Manispaa hiyo sambamba na kukata keki,na kuimba nyimbo mbalimbali za kumtakia maisha marefu Rais Samia.

Pia uongozi wa shule hiyo kupitia kwa mwalimu mkuu wa shule  Juliana Rukweto  alisema kuchaguliwa shule hiyo, imeongeza imani kwao kuwa wanathaminiwa katika jamii  pia ni njia ya kuwatia  moyo wa kuendelea kufanya vizuri katika masomo yao.

 Aidha Rukweto amewashukuru vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo kwa kuonyesha mwitikio  wa kujitokeza kupanda miti na  kuichagua shule hiyo kuwa Sehemu ya kusherekea sikukuu hiyo ya kuzaliwa na kubaki na kumbukumbu.

Kwa upande wao, baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Omunwani,Brandina Conrad,Diana Wilbroad na Tausi Kassim wameishukuru Jumuiya ya Vijana wa Kagera kwa kutoa miche 2,000 ya miti kwa ajili ya kuboresha mazingira ya shule hiyo.

Walisema upandaji wa miti una faida nyingi ikiwemo kuboresha mazingira ya kujifunzia, kivuli na hewa safi, huku wakiahidi kuitunza miti hiyo hadi ikue kama sehemu ya kumbukumbu ya kusherekea miaka 66 ya Rais

‎Naye Mhifadhi Misitu wa Wilaya ya Bukoba Anatory Lagweni amewahimiza wananchi kupanda miti ya aina mbalimbali katika makazi yao na maeneo ya wazi, akisisitiza umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika juhudi za kuhifadhi mazingira na misitu kwa maendeleo ya sasa na baadaye.












Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top