Fahamu Kuhusu Malipo ya Pensheni ya Mkupuo Kwa Wastaafu Waliostaafu kwa Umri na Ugonjwa Kutoka PSSSF.

0

 


Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeanza kutoa pensheni ya mkupuo ya miezi 36 kwa wategemezi wa wastaafu waliostaafu kwa umri au ugonjwa pekee, hatua ambayo inalenga kuhakikisha familia za wastaafu zinapata usaidizi wa kifedha baada ya kifo cha mstaafu.

Kwa mujibu ya taarifa katika jarida maalum la PSSSF, mfuko huu unatoa huduma mbalimbali za mafao, ikiwemo mafao ya muda mrefu kama vile uzeeni, ulemavu na mirathi, pamoja na mafao ya muda mfupi kama vile mafao ya uzazi, ukosefu wa ajira na ugonjwa. Pensheni ya mkupuo ni huduma mpya iliyoanza kutolewa kuanzia Januari 1, 2025, kwa wastaafu waliostaafu kwa umri au ugonjwa tu.

Vigezo vya Kunufaika

Malipo ya pensheni ya mkupuo yanapatikana kwa wategemezi wa mstaafu aliyefariki aliyekuwa akilipwa pensheni, na ni kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko, Kifungu cha 39 (1) na (2). Wategemezi wanaostahili ni:

  • Mjane au mgane wa mstaafu
  • Malipo yanalipwa kwa wategemezi wa mstaafu wa umri/ugonjwa aliyekuwa akilipwa na pensheni
  • Wategemezi wanaostahili kulipwa ni kwa mujibu ya sheria ya mfuko, kifungu cha 39 (1) na (2). Mjane/mgane au watoto walio chini ya miaka 18 (miaka 21 ikiwa bado wapo shuleni
  • Malipo kwa wategemezi yatalipwa kufuatia kifo cha mstaafu aliyefariki dunia kuanzia tarehe 01, Januari, 2025 au alilipwa mafao kwa kanuni mpya iliyoanza kutumika tarehe 01,Julai 2022
  • Malipo haya yatakuwa ni sawa na pensheni ya miezi 36 ya mstaafu husika wa umri/ugonjwa ambaye amefariki
  • Pensheni itakayotumika kulipia pensheni ya Mfuko peke yake iliyokokotolewa kwa kuzingatia kipindi/vipindi vyake vya utumishi.
  • Malipo yote ya pensheni yaliyolipwa baada ya mstaafu kufariki, yatafidiwa kutoka kwenye mkupuo wa pensheni ya miezi 36.
  • Malipo haya yatafanyika mara moja kwa kila mstaafu aliyefariki.Mgawanyo wa malipo haya utafanyika kwa mujibu wa kanuni ya mafao ya PSSSF 17 (2) na (3)
  • Malipo haya yatafanyika kwa pamoja kwenye daftrari la pensheni ya kila mwezi.

Malipo haya yatakuwa sawa na pensheni ya miezi 36 ya mstaafu aliyefariki, na yatafanyika mara moja kwa kila mstaafu aliyefariki. Mgawanyo wa malipo utafanyika kwa mujibu wa Kanuni ya Mafao ya PSSSF 17 (2) na (3), na yataonyeshwa kwenye daftrari la pensheni ya kila mwezi.

Utendaji wa Malipo

  1. Malipo yataombwa kupitia mtandao.
  2. Msimamizi wa mirathi atatakiwa kufika kwenye ofisi ya mfuko kutoa taarifa za kifo cha mstaafu na kuwasilisha nyaraka zifuatazo:
    • Nakala iliyothibitishwa ya cheti cha kifo cha mstaafu
    • Namba ya pensheni au cheki namba ya mstaafu
    • Nakala ya fomu ya mahakama ya uteuzi wa usimamizi wa mirathi
    • Kitambulisho cha NIDA au Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN)
  3. Baada ya msimamizi kusajiliwa kwenye mfumo wa mfuko, ataweza kuanzisha dai la malipo kwa mtandao popote alipo.
  4. Nyaraka zinazohitajika wakati wa kuanzisha dai ni:
    • Fomu maalum ya maombi ya mafao ya mkupuo wa pensheni “Ben.15
    • Nakala iliyothibitishwa ya cheti cha ndoa (ikiwa marehemu alikuwa ameoa/kuolewa)
    • Nakala zilizothibitishwa za vyeti vya kuzaliwa vya watoto
    • Fomu ya “Ben.10” iliyojazwa kikamilifu na kuthibitishwa na benki/mahakama
    • Taarifa za benki za wategemezi
  1. Mfuko utapokea dai lililotumwa na kulifanyia kazi, huku taarifa zote za maendeleo ya dai zikionekana mtandaoni.

📷Picha na maelezo kwa hisani ya PSSSF

✍️imeandikwa na Emmanuel Chibasa

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top